MKUU wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na maafisa wa polisi mkoa wa Mbeya wakiangalia mazoezi ya kikosi cha FFU Mbeya |
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiongea na kikosi cha FFU Mbeya |
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amelitaka Jeshi la Polisi kujifunza mbinu mbali mbali za kukabiliana na majambazi kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo katika jamii na kuhatarisha usalama wa raia. |
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema utaratibu wa kufanya
mazoezi kwa askari wa kupambana na kutuliza ghasia hufanyika mara mbili
kwa wiki ikiwa na lengo la kuangalia hali ya nidhamu, ukakamavu na
utayari wa Askari katika kupambana na uhalifu.
|
Mazoezi yakiendelea |
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amelitaka Jeshi la Polisi kujifunza
mbinu mbali mbali za kukabiliana na majambazi kutokana na kukithiri kwa
vitendo hivyo katika jamii na kuhatarisha usalama wa raia.
Aidha
aliwataka Wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi na Vyombo vya
ulinzi ili kudumisha amani na utulivu kwa kushiriki kutoa taarifa za
uhalifu pamoja na ulinzi shirikishi kwa kutii sheria bila shuruti.
Kandoro
alitoa kauli hiyo alipotembelea mazoezi ya Askari wa Kutuliza
ghasia(FFU) mkoani hapa katika viwanja vyao mazoezi yenye lengo la
kudumisha nidhamu, ukakamavu na utayari wa kukabiliana na adui kwa
Askari wa Jeshi la Polisi.
Alisema
jeshi la Polisi pekee haliwezi kudumisha hali ya amani na utulivu kwa
Watanzania bila kupata ushirikiano kutoka kwao kwa kutoa taarifa pindi
wanapobaini kuwepo kwa hali ya hatari ama uhalifu katika maeneo yao.
Aliongeza
kuwa Jeshi la Polisi linatakiwa kuongeza kasi ya kutoa elimu kwa
wananchi juu ya utii wa sheria bila shuruti pamoja na ulinzi shirikishi
jambo litakalosaidia kupunguza vurugu zisizokuwa na msingi katika jamii.
Alisema
pia wananchi hawapaswi kulazimisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa
katika kukabiliana nao kutokana na kushindwa kutii amri zinazotolewa na
kukatazwa jambo bali watumie njia ya mazungumzo wanapokuwa na madai na
siyo kukimbilia kufunga barabara na kuchoma moto.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema
utaratibu wa kufanya mazoezi kwa askari wa kupambana na kutuliza ghasia
hufanyika mara mbili kwa wiki ikiwa na lengo la kuangalia hali ya
nidhamu, ukakamavi na utayari wa Askari katika kupambana na uhalifu.
Katika
mazoezi hayo Askari waliweza kumuonesha Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa mbinu mbali mbali za kukabiliana
na maadui ikiwa ni pamoja na kudhibiti vurugu kwa kutumia mbinu mbali
mbali, kukabiliana na majambazi wenye silaha pamoja na mbinu za kivita.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|