Mh
Aikael Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa UKAWA kutoka nje ya bunge
maalumu la katiba na kutorudi tena bungeni bali kwenda kwa wananchi.
Mheshimiwa
Mbowe ameeleza jinsi ambavyo bunge linavyoendeshwa kwa upendeleo mkubwa
sana,Matusi makubwa ya nguoni kwa wajumbe wenye mawazo tofauti na ya
serikali ya ccm,kutumia vitisho vingi,udhalilishaji na uonevu mkubwa .
Mheshimiwa Mbowe ametolea mfano
kwamba Kama Lukuvi amekwenda kanisani na kuanza kuhutubia watu kwamba
kama serikali 3 zitapita Jeshi litachukua nchi.Hivi ni vitisho ambavyo
kwanza vinampunguzia umakini ama uwezo rais aliyepo madarakani na pia ni
kuamsha hisia za jeshi kufanya hivyo hata leo.Kwa maneno mengine ni
kuwapa mawazo ama maoni wanajeshi wetu kupindua serikali.
Inashangaza sana Mheshimiwa Lukuvi hawezi kuwajibika kwa kauli hii
kwani mwaka 2009 Samson Mwigamba aliwahi kuandika makala fulani kwenye
gazeti la TANZANIA DAIMA kuhusu jeshi lakini serikali ya ccm
ikamfungulia mashtaka mahakamani kwamba ni mchochezi na analitaka jeshi
LIASI TAIFA NA KUFANYA MAPINDUZI ( ARMY MULTINY AND REVOLUTION) na
bahati nzuri sana kesi ile Mwigamba alishinda mwezi Fenruary 2014.Je
serikali haioni kwamba Lukuvi ameamsha hisia na kufanya uchochezi jeshi
kuasi????
Hata hivyo,mimi binafsi nadhani ccm wanakiinimacho wananchi.Wananchi
wamesema Wanataka serikali 3 wao wanatoa vitosho vya Muungano
kuvunjika,wanatoa vitisho kwamba nchi itaingia vitani,wanatoa vitisho
kwamba fanya ufanyalo ni serikali 2 tu na mwingine akasema kwamba hata
kama wananchi wanataka serikali 3 basi wasubiri yeye aondoke madarakani
kwanza.