Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akiteta jambo na
baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa toleo jipya
la gari aina ya Mercedes Benz E-Class uliofanyika jijini Dar kwenye
hoteli ya Capetown Fish Market.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (wa pili kulia)
na Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed (wa pili kushoto)
wakibadilishana mawazo na wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi
wa toleo jipya la Mercedes Benz E-Class uliofanyika kwenye hoteli ya
Capetown Fish Market jijini Dar.(Picha na Zainul mzige)
Wanenguaji wa kizungu wa Maendeleo Dance Group wakiburudisha tukio hilo la uzinduzi wa toleo jipya la Mercedes Benz E-Class jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania, Wayne McIntosh akizungumza
na wageni waalikwa katika uzinduzi wa gari hiyo mpya katika soko la
Tanzania kwenye hoteli ya Cape Town Fish Market Msasani jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Wayne McIntosh, akizindua rasmi
Mercedez Benz aina ya E-Class jijini Dar esSalaam kwenye hafla fupi
iliyofanyika kwenye hoteli ya Capetown Fish Market.
Sasa imezinduliwa rasmi katika soko la Tanzania.
Toleo jipya la gari aina ya Mercedes Benz E-Class lililozinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam na kampuni ya CFAO Motors.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo la kipekee.
Mmoja wa wageni waalikwa akionekana kuvutiwa na toleo jipya la Mercedes Benz E-Class.
Mwakilishi
wa TV 1 kutoka nchini Ghana akipozi na gari matata aina ya Mercedes
Benz E-Class kwenye hafla fupi ya uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa juma
jijini Dar.
Muonekano wa ndani wa gari hilo lenye speed 260.
Mmoja wa models aliyepamba uzinduzi huo akipozi kwenye toleo jipya la Mercedes Benz E-Class.
Muonekano wa nyuma.
Mkurugenzi
Mkuu wa benki ya Wanawake Tanzania, Bi.Margareth Chacha akifanyiwa
mahojiano na TV1 ambapo akielezea mapenzi yake na magari ya aina ya
Mercedes Benz ambapo hapo awali alikuwa akitumia na panapomajaliwa ya
Mungu siku moja atamiliki toleo jipya la Mercedes Benz E-Class.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Tharaia Ahmed akisalimiana na
Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Wanawake Tanzania, Bi.Margareth Chacha
kwenye hafla hiyo. Katikati ni Hellen Kiwia kutoka Frontline Management.
Meneja
Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed akifafanua jambo kwa mmoja wa
wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa toleo jipya la Mercedes Benz
E-Class.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Wayne McIntosh, akisalimiana na
mmoja wa wageni waalikwa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Wanawake Tanzania,
Bi.Margareth Chacha (kushoto) kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa
toleo jipya la Mercedes Benz E-Class. Katikati ni Tender Manager wa CFAO Motors Bw. Marco Kahabi.
Crew ya stesheni mpya ya TV 1 nao waliokuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.
KAMPUNI ya CFAO Motors Tanzania hivi karibuni wamezindua gari mpya
aina ya Mercedes-Benz E-Class Saloon na Estate yenye muonekano bora
zaidi na inaweza kutembea bila dereva amesema Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo.Akizungumza na wageni waalikwa jijini Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa gari hilo la Meredes-Benz, E-Class, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania, Wayne McIntosh amesema gari hiyo nia aina mpya kabisa na kisasa zaidi kutengenezwa na kampuni hiyo.
“wakati wa majaribio nchini Ujerumani gari hii iliweza kutembea kilometa kadhaa bila kuwa na dereva kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu kabisa,” amesema McIntosh.