Wananchi
hao kutoka Kijiji cha Kibande na vijiji viongine wilayani Buhigwe,
Kigoma Tanzania, huenda Burundi kufanya biashara kutokana na upande wa
Tanzania kutokuwepo na soko kunakosababishwa na kodi nyingi.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni
mpaka wa Tanzania na Burundi, alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe
mkoani Kigoma,Kinana yupo katika ziara ya siku 5 mkoani humo ya
kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa
kwa kufuata Ilani ya CCM.
Hizi
ni baadhi ya picha zinazoonesha jinsi wananchi wa Tanzania wakivuka mto
huo na wengine kuvushwa kwa malipo, wakirudi Tanzania baada ya kufanya
biashara upande wa Burundi.
Watu
wote hao wakisubiri kuvushwa kwenye mto huo Malagalasi,kwa kimtumbwi
kimoja ama kubebwa kama baadhi ya picha zinavyoonyesha Baadhi ya
Wanahabari pichani Kulia Bakari Kimwanga kutoka gazeti la Mtanzania na
Bwana Jongo kutoka gazeti la Uhuru wakionja joto ya kuvushwa kwenye mto
wa Malagalasi ambao ndio sehemu ya mpaka kati ya Burundi na Tanzania.
Kuonja
adha hiyo hulipia kiasi cha fedha shilingi 500 mpaka 1000 kama nauli.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo kwa msisitizo na
Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Buhigwe,Kaondo Julius
walipokwenda kukagua mpaka wa Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara
wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
Msanii
wa kikundi cha ngoma za utamaduni kutoka Burundi wakitumbuiza katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kibande, Wilaya ya Buhigwe
mkoani Kigoma. Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Makamu
Mwenyekiti wa chama cha CNDD-FDD,Mkoa wa Makamba nchini Burundi,Bwa.
Nishimwe Zen,kabla ya mkutano wa hadhara kufanyika katika kijiji cha Kibande,wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.