MBEYA CITY COUNCIL FOOTBALL CLUB
TAARIFA KWA UMMA
UPOTOSHAJI UNAOTOLEWA DHIDI YA TIMU YETU KUELEKEA MCHEZO WA TAREHE 13/4/2014
Kwanza
nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo wa
mpira wa miguu na wapenzi wa Mbeya City Fc popote pale walipo kwa
kuiunga mkono timu yao muda wote wa michezo ya ligi kuu inayoelekea
ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini nafasi ya wapenzi na washabiki
katika kujenga timu imara na yenye ushindani kama walivyofanya kwa timu
yetu.
Timu
yetu ilianza ligi msimu huu 2013/2014 ikiwa na malengo ya kuchukua
ubingwa au kuwa katika nafasi za juu za ligi yetu.Hiyo ndiyo dhamila
iliyokuwepo kwa viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Michezo
miwili imesalia kwa timu yetu kabla ligi kuu ya Vodacom kumalizika
katika msimu huu 2013/2014.katika safari yetu ya ligi kuu kwa mara ya
kwanza msimu huu, changamoto nyingi za kiutawala na za kimtazamo kutoka
kwa wadau wote wanaohusika na mchezo wa mpira wa miguu nchini
tumezishuhudia .Changamoto hizo ni ikiwemo upangaji wa ratiba usiyokuwa
na uwiano mzuri,baadhi ya mechi kuamuliwa vibaya na waamuzi wa
mchezo,wizi wa mapato ya milangoni unaotokana na mfumo mbaya wa uuzaji
wa tiketi,uadilifu mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana ya
kusimamia mpira katika ngazi zote n,k.
Kuelekea
mchezo wetu wa tarehe 13/04/2014 dhidi ya AZAM FC kumezuka propaganda
chafu na ambazo si sahihi katika ukuzaji wa mpira hasa wa ligi ndogo
kama ya Tanzania. Nachukua nafasi hii kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo
ambayo yamekuwa sehemu ya propaganda hizo:
1. Klabu
imehaidiwa kununuliwa basi na hivyo inajiandaa kutoa ushindi kwa kwa
timu ya AZAM Fc na kuwarahisishia mazingira ya Ubingwa.
Halmashauri
ya jiji la Mbeya limekuwa katika mchakato wa kutafuta na kununua basi
kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Halmashauri ikiwemo kutumiwa na
timu zake ( Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo ligi kuu ya
michezo husika kwa kufuata sheria ya manunuzi ya Umma. Mchakato huo
ulianza tarehe 8/8/2013 halmashauri ilipotangaza nia hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe hiyo kwa tender no.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 hii
ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo yake ya
ndani kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
Tangazo
hilo halikupata mzabuni mwenye sifa za kufanya usambazaji wa basi hilo
hivyo tangazo hilo lilirudiwa tena tarehe 12/2/2014 katika gazeti la
majira kwa Tender No.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 (Re-advitised), Mchakato na maandalizi ya ufunguaji wa ufanyaji wa tathmini wa zabuni hiyo unaendelea kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma.
Pamoja
na mchakato huo hapo juu,pia klabu inaendelea na mazungumzo na wadau
mbalimbali wenye nia ya kuwekeza kwa udhamini wa bidhaa zao,moja ya
maeneo ya udhamini ni pamoja na ununuzi wa basi la wachezaji taratibu
na makubaliano haya yatakapo kamili umma wa wapenda mchezo wa mpira wa
mguu utajulishwa.
Hivyo propaganda hiyo kuwa klabu imehongwa basi si za kweli na si sahii ila zina nia ya kuidhalilisha timu yetu.
2. Propaganda
kuwa Mwalimu Juma Mwambusi kanunuliwa nyumba Maeneo ya chamazi ili
apange kikosi dhaifu siku ya mchezo tarehe 13/4/2014.
Mwalimu(Kocha)
Juma Mwambusi ni muajiliwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya,kwa maana
hiyo ni mtumishi wa Umma. Mwalimu Mwambusi amekuwa na timu yetu kwa muda
mrefu sasa na ataendelea kuwepo.Kumekuwepo na maneno yasiyofaa dhidi ya
mwalimu wetu toka mzunguko wa pili wa ligi kuanza,maneno haya yamekuwa
na nia ya kuaribu muenendo wa timu ili ianze kufanya vibaya lakini zaidi
ya hapa yana nia ya kumdhalilisha mwalimu wetu na taaluma ya ukocha
nchini.
Mwalimu amefedheheshwa sana na taarifa hizo.
3. Propaganda kuwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wamepewa hongo wacheze chini ya kiwango 13/4/2014.
Wachezaji
ndiyo wachezaji wenye nidhamu kubwa katika ligi ya mwaka huu ndani na
nje ya uwanja muda wote,ni waadirifu na wanajua wanataka nini.Mpira
ndiyo ajira yao kama watumishi wa umma ndani ya Halmashauri ya jiji la
Mbeya.Hawajawahi na wala hawatawahi kuchukua rushwa kwa lengo la kupanga
matokeo.
Klabu
yetu haisadiki katika upangaji wa matokeo ya mchezo wa mpira wa miguu
kwani tunajua fika kuwa hakutaisadia kama klabu lakini pia kama taifa
katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Hitimisho,
Mchezo
wa mpira wa miguu una matokeo matatu kushinda,kushindwa na kutoka sare.
Klabu inaamini kuwa timu iliyojiandaa vizuri kama yetu inastahili
kupata matokeo mazuri uwanjani.Falsafa mojawapo ya timu yetu ni kushinda
mechi kwa kucheza mpira unaovutia na kuwaburudisha watazamaji.
Tuhuma
mbalimbali za upangaji matokeo katika ligi yetu zimeanza kuota mizizi
hasa ligi inapoingia mzunguko wa pili ,katika suala hili kama ambavyo
linataka kuhusishwa nasi yawezekana propaganda hizi kwa upande wa timu
inayotuhumiwa kuandaa michakato hiyo wana uzoefu nalo na yumkini ndiyo
chachu ya mafanikio yao mpaka kufikia hatua hiyo waliofikia sasa.
Kama
timu hiyo inauwezo wa kirasilimali wa kufanya uovu huo wote iweje
ishindwe kuwa na timu imara na ya ushindaji mpaka itegemee kutafuta
wachezaji wa timu pinzani kupata matokeo mazuri?
Timu
yetu ndiyo timu pekee changa miongoni mwa timu tano zinazoongoza
msimamo wa ligi yetu kwa sasa,si hivyo tu bali ndiyo timu pekee
inayoundwa na wachezaji wengi wapya katika ulimwegu wa soka na
inayoundwa na Watanzania watupu kuanzia wachezaji,benchi la ufundi
pamoja na viongozi.Hii inathibisha kuwa kama taifa tunaweza kufanya kazi
nzuri bila kutegemea wachezaji toka nje baadhi yao wasiokuwa na tija.
Mpira
ni ajira hatuna budi kuuratibu vema ili kutoa nafasi inayostahili kwa
vijana wetu ili kupunguza tatizola ajira nchini lakini pia kutumia
vipaji vyao kulipa taifa muonekano stahili.
Mamlaka
zinazohusika hazina budi kuanza kufuatilia na kuchukua hatua kali kwa
baadhi ya timu zinzohusishwa na upangaji wa matokeo ili kulinda heshima
ya mchezo huo bila kuogopa uwezo wa rasilimali wa timu hizo.
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
9.04.2014