YANGA YACHOMOA DAKIKA ZA MWISHO NA KULAZIMISHA SARE YA 1-1 DHIDI YA MNYAMA SIMBA SC!!

Kinachoendelea hapa ni utoaji wa zawadi kwa mshindi wa pili

FT: YANGA SC 1 : 1 SIMBA SC

Mpira umekwisha uwanja wa Taifa.

Dakika za majeruhi, Simba wanashambulia kwa nguvu
90+5
Dakika 90` zimeshakatika na zimeongezwa dakika 5.

Kuna shabiki mwingine kwa upande wa Yanga anaanguka hapa.

Kuna shabiki wa Simba amezirai baada ya kusawazishwa kwa bao, watu wa huduma ya kwanza wanakwenda kumsaidia.

Dakika za lala salama, Dida yuko chini anafunga viatu vyake, huku makocha wa Yanga wakiwaelekeza wachezaji nini cha kufanya.

Dakika ya 86` Saimon Msuva anaisawazishia Yanga bao kwa shuti kali  baada ya mabeki wa Simba kushangaashangaa , matokeo 1-1.

Simba wanafanya mabadiliko, Singano anatoka anaingia Juma Awadh.
NKoch msaidizi wa Simba, Suleiman Matola na kocha wa makipa Idd Pazzi wanatolewa kwa kadi nyekundu, Loga amebaki peke yake.

Dakika ya 36` Simba wanaongoza kwa bao 1-0.

Nje kidogo ya eneo la hatari la Simba Ngassa anawekwa chini na Kiemba na kuwa faulo, lakini Domayo anapiga mpira unaokuwa goli kiki.
Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Hamis Kiiza anaingia Hussein Javu.

Dakika ya 31` kipindi cha pili, Haruna Chanongo inaipatia Simba sc bao la kuongoza baada ya Kipa Dida kuutema mpira wa krosi uliochongwa na Lucian na kumkuta Chanongo anayeachia shuti kali.

Hussein Javu anapiga jalamba kwa muda mrefu.

Yanga wanataka hapa uwanjani na kuwaweka nusu uwanja Simba

Dakika ya 26` kipindi cha kwanza shabiki mmoja ameingia uwanjani na kuiba taulo la Ivo, lakini amekamatwa na polisi.

Dakika ya 25` kipindi cha pili Kona inapigwa kuelekea lango la Simba lakini Mosoti anaokoa.

Dakika ya 25` kipindi cha pili, Ivo Mapunda amesimama na anatumia taulo lake kujifuta.

Ilikuwa hatari langoni mwa Simba baada ya Msuva kupiga shuti kali , lakini Donald Mosoti ameokoa na Ivo Mapunda anagaagaa langoni.

Cholo naye anakwenda benchi nafasi yake inachukuliwa na Wiliam Lucian `Gallas`.

Simba wanafanya mabadiliko, Uhuru Seleman Mwambungu  ameingia kuchukua nafasi ya Said Khamis Ndemla.

Kona inapigwa na Saimon Msuva, naona mwamuzi hajaamuru ipigwe.
Mpira umesimama hapa kwa jambo la kipuuzi. Taulo lingine linawekwa na Kavumbagu anaoneshwa kadi ya njano.
Wachezaji wa Yanga wanaonesha imani ya kishirikina kwa kudhani Taulo la Ivo linazuia mabao.
Didier Kavumbagu anatoa taulo la Ivo Mapunda langoni na kulitupa kwa mashabiki wa Yanga
Saimon Msuva anaingiza krosi hatari lakini Simba wanaokoa na inakua kona.
Dakika ya 10` kipindi cha pili Kona inapigwa na Msuva kuelekea lango la Simba, lakini kipa Mapunda anadaka mpira.
Dakika ya 7` kipindi cha kwanza, Oscar Joshua anamfanyia madhambi Singano na mpira ni faulo, lakini mabeki wa Yanga wanaokoa.
Dakika ya 5` kipindi cha pili Simba wanafanya shambulizi kali baada ya Cholo kupiga shuti kali mno, lakini Dida anaonesha umahiri langoni.
Dakika 4` kipindi cha pili zimekatika milango bado ni migumu
Mpira umeshaanza hapa uwanja wa Taifa
Waamuzi wanaingia kumalizia dakika 45` za kipindi cha pili.
Kikosi cha Simba sc kimeshaingia uwanjani, lakini Yanga wapo kwenye vyumba vya kuvalia nguo.
Kipindi cha pili kinatarajia kuanza hivi punde tu.
HT: YANGA SC 0 : 0 SIMBA SC
Dakika 45` za kipindi cha kwanza zimetimia na inaongezwa dakika moja. Dakika ya 44` kipindi cha kwanza Cholo anazawadiwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Msuva  na inakuwa faulo kupigwa kueleka lango la Simba nje kidogo ya eneo la hatari. Ngassa anakosa.
Dakika ya 43` kipindi cha kwanza Said Ndemla anakosa bao baada ya kupata kigugumizi cha kichwa kufuatia krosi iliyochongwa na Haruna Chanongo.
Dakika ya 43` kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mwenzake. Dakika ya 40` kipindi cha kwanza kasi ya mpira imepungua hapa uwanjani. Dakika ya 39` kipindi cha kwanza, si Simba wala Yanga aliyeona lango la mwenzake.
Yanga wanapata kona lakini Ivo Mapunda anaokoa na kuanguka chini, amepata maumivu.
Dakika ya 34` kipindi cha kwanza, Ngassa anaingia langoni mwa simba na kukosa bao baada ya Ivo Mapunda kusimama imara.
Dakika 33` za kipindi cha kwanza zimeshakatika mpaka sasa, Simba wanatawala zaidi mpira na kufanya mashambulizi ya nguvu
Dakika ya 32` kipindi cha kwanza Simba wanafanya shambulizi la nguvu langoni mwa Yanga, lakini Amiss Tambwe anakosa bao.
Dakika ya 30` kipindi cha kwanza Said Ndemla anamjaribu kipa Deo Munish `Dida` kwa kupiga shuti kali.
Dakika ya 29` kipindi cha kwanza Amiss Tambwe anafanyiwa madhambi na Yondani nje kidogo ya eneo la hatari, lakini mabeki wanaokoa.
Dakika ya 29` kipindi cha kwanza Piga nikupige langoni mwa Yanga, Mpira hautaki kuondoka.
Dakika ya 28`  kipindi cha kwanza Simba wanafanya shambulizi lakini Yondani anatoa mpira na kuwa kona inayookolewa na mabeki wa Yanga.
Dakika 26` kipindi cha kwanza Yanga wanashambulia lango la Simba lakini kichwa cha Didier Kavumbagu kinakosa macho.
Dakika 25` kipindi cha kwanza Simba wanapeleka shambulizi la hatari langoni mwa  Yanga lakini mabeki wa Yanga wanaokoa
Dakika ya 24` kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mwenzake. Dakika ya 22` kipindi cha kwanza Yanga wanapata kona inayochongwa na Saimon Msuva  lakini Mkude anaokoa.
Dakika ya 14` Simba wanapata kona na inapigwa na Singano, lakini inawababatiza mabeki wa Yanga na kuwa kona ya pili hata hivyo haizai matunda.
Dakika ya 10` kipindi cha kwanza milango bado migumu
Dakika ya 7` kipindi cha kwanza milango bado ni migumu

Dakika ya 4` kipindi cha kwanza Simba wanapata kona Yanga wanaokoa.
Mpira umeshaanza hapa uwanja wa Taifa.
Mashabiki ni wachache sana tofauti na mechi za nyuma.

YANGA 1 : 1 SIMBA SC
.....................................................................
KIKOSI CHA YANGA SC
 Here's Young Africans line-up to face Simba Sc today:
1. Deo Munish "Dida" - 30
2. Mbuyu Twite - 6
3. Oscar Joshua - 4
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23
5. Kelvin Yondani - 5
6. Frank Domayo - 18
7. Saimon Msuva - 27
8. Hassan Dilunga - 26
9. Didier Kavumbagu - 7
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamis Kizza - 20

Subs:
1. Barthez, 2.Job, 3. Zahir, 4.Telela, 5.Nizar, 6. Javu, 7. Jerson Tegete


KIKOSI CHA SIMBA SC

1. Ivo Mapunda
2. Masud Nassoro `Cholo`
3. Issa Rashid `Baba Ubaya`
4. Joseph Owino
5. Donald Mosoto
6. Jonas Mkude
7. Haruna Chanongo
8. Said Ndemla
9. Amis Tambwe
10. Amri Kiemba
11. Ramadhan Singano `Messi`.

SUB
1. Yaw Berko
2. Wiliam Lucian `Gallas`
3. Henry Joseph
4. Uhuru Seleman Mwambungu
5. Ramadhan Chombo `Redondo`
6. Zahor Pazzi



CREDIT:-MPENJA BLOG


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...