Eto’o amerudia tena staili ya kuonesha uzee wake baada ya kufunga bao na haya bado ni majibu kwa Mourinho.MSHAMBULIAJI
mkongwe, Samuel Eto`o jana usiku aliifungia bao la kuongoza timu ya
taifa ya Cameroon katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kujiandaa na
fainali za kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani.
Katika
mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 2-2, mkongwe huyo mwenye miaka 33
alifunga bao dakika ya 62 na kushangilia kwa `staili` yake ya kikongwe
anayetembelea mkongojo.
Ikumbukwe
aliwahi kushangilia kwa `staili` hiyo wakati alipoifungia Chelsea bao
ikiwa ni kejeli kwa kocha wake, Jose Mourinho aliyekuwa anambeza kuwa
kwasasa Mcameroon huyo amezeeka.
Eto’o,
aliingia katika vita ya maneno baada ya maneno hayo ya kejeli kutoka
kwa Mourinho aliyehoji umri wake sahihi mapema mwanzoni mwa msimu, na
baada ya kufunga jana alikimbilia sehemu ya kibendera cha kona na
kushangilia kwa staili yake ya comedi inayoonesha uzee wake.
Kikosi
cha Ujerumani: Weidenfeller, Boateng, Mertesacker, Hummels, Durm
(Howedes, 85), Khedira (Kramer, 73), Kroos, Muller, Ozil (Podolski, 63),
Reus, Gotze (Schurrle, 58).
Wachezaji wa akiba: Zieler, Grosskreutz, Schmelzer, Schweinsteiger, Klose, Mustafi, Draxler, Ginter, Volland.
Wafungaji wa magoli: Muller, 66, Schurrle, 71.
Aleyoneshwa kadi ya njano: Boateng. Kikosi cha Cameroon: Itandje, Djeugoue, Bedimo (Assou-Ekotto, 58), N’Koulou, Song, Mbia (N’Guemo, 46), Enoh, Matip, Choupo-Moting, Moukandjo, Eto’o (Webo, 90). Wachezaji wa akiba: N’Djock, Kana Biyik, Nounkeu, Aboubakar, Makoun, Chedjou, Idrissou, Bong Songo, Nyom, Salli, Olinga, Loe.
Wafungaji wa magoli: Eto’o 62, Choupo-Moting, 78.
Aliyeoneshwa kadi ya njano: Song, Enoh.
Mwamuzi: Damir Skomina (Slovenia)

Nyota
huyo wa zamani wa Barcelona na Inter alifunga bao la kwanza lakini
dakika chache baadaye Thomas Muller aliunganisha krosi nzuri ya Jerome
Boateng na kusawazisha bao hilo.
Wenyeji waliandika bao la kuongoza kupitia kwa nyota wa Chelsea Andre Schurrle baada ya kutumia vyema pasi ya Lukas Podolski.
Hata hivyo bao hilo halikudumu baada ya Eric Maxim Choupo-Moting -kuisawazishia Cameroon.