Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, limelazimika kuwaita wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kushuhudia mwili wa mtu aliyekutwa amekufa kwenye kichaka jirani na ofisi za makao makuu ya jeshi hilo.
Kwa
mujibu wa polisi, mwili wa mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Juma
Mbega (46) ulikutwa kwenye kichaka ukiwa umeharibika vibaya na kutoa
harufu kali huku ukizungukwa na wadudu, nusura polisi wenyewe watoke
nduki.
Akizungumza
na mwanahabari wetu, Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro,
Afande Suzy alisema wakiwa ofisini, walisikia harufu kali hivyo
kulazimika kufanya uchunguzi ndani na nje ya jengo hilo la polisi lenye
ghorofa moja ambapo chini zipo ofisi za Jeshi la Polisi Wilaya ya
Morogoro Mjini na juu za mkoa.
alisema afisa huyo.
Kwa upande wake, Nuru Adam ambaye ni mjomba wa marehemu huyo, akizungumza na gazeti hili eneo hilo la tukio alisema:
Baada
ya uchunguzi wa awali na ndugu wa marehemu kujulikana, maiti
ilichukuliwa na kupelekwa mochwari kuhifadhiwa huku taratibu za mazishi
kwa ndugu zikiendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.