ISHARA za mwisho wa dunia? Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb amekula kichapo na kuishia mikononi mwa polisi baada ya kunaswa katika nyumba ya kulala wageni (gesti) akiwa na dogo wa kiume aliyedaiwa kuwa ni denti wa sekondari.
Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb akiwa amepigw pingu baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kiume gesti.
Aibu hiyo
ya karne ilijiri juzi Jumatatu kwenye gesti hiyo (jina linahifadhiwa)
iliyopo maeneo ya Manzese, Dar ambapo jamaa huyo alikutwa chumbani na
denti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 14.
Kwa
mujibu wa chanzo makini kilichoitonya Timu ya Oparesheni Fichua Maovu
(OFM) ya Global Publishers, njemba huyo amekuwa na ‘katabia kachafu
kakuwafanyia usodoma’ watoto wa kiume.Habari hizo zilidai kuwa ishu hiyo
iliwakera wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu
ndipo wakaamua kumfungia kazi baada ya kudaiwa kuwa na mtoto huyo
chumbani usiku kucha.
Kwa
mujibu wa meneja wa gesti hiyo (aligoma kuta jina) ambaye alitoa
ushirikiano wa kutosha kwa OFM, raia hao walikuwa wakimchunguza njemba
huyo kwa muda mrefu kutokana na tabia ya kulala kwenye gesti hiyo na
watoto wa kiume.
Njemba aliyekutwa na denti akipanda kwenye difenda.
“Mwanzo
tulifikiri anakuja na vijana hao kama marafiki zake wa kawaida lakini
tukaingiwa na wasiwasi baada ya kugundua kuwa alikuwa akilala nao kwa
kuwabadilisha,” alisema meneja huyo.
Alidai kwamba Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 usiku, kijana huyo alitinga tena kwenye gesti hiyo lakini alikuwa peke yake na kupewa chumba kama kawaida.
Alidai kwamba Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 usiku, kijana huyo alitinga tena kwenye gesti hiyo lakini alikuwa peke yake na kupewa chumba kama kawaida.
“Wahudumu
waliniambia kuwa jamaa amefika tena na amechukua chumba cha juu lakini
safari hii alifika peke yake, ilinishangaza sana kusikia kaja peke yake
kwani siyo kawaida yake so sikuamini,” alieleza meneja huyo.
Alidai
kwamba asubuhi ya Jumatatu, mishale ya saa 4:00, wahudumu walisikia
miguno ndani ya chumba alicholala njemba huyo ndipo wakakifunga kwa nje
kisha kuita polisi na vijana wa OFM ambao walifika eneo la tukio ndani
ya ‘dakika sifuri’.
Meneja
huyo alisema kuwa hafahamu njemba huyo alimuingiza kijana huyo muda gani
kwani walimuwekea mtego siku nyingi akawa anachezwa na machale.
Hata
hivyo, Jiji la Dar huwa halina dogo kwani wakazi wa eneo hilo walijazana
kwenye gesti hiyo kutaka kumpiga jamaa huyo lakini polisi walifanikiwa
kuwatorosha eneo hilo na kuwampeleka Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar.
Hadi OFM
inang’oa nanga kituoni hapo, njemba huyo na kijana aliyekutwa naye
walikuwa wakiendelea kuhojiwa. Kujua kilichojiri usikose kufuatilia
magazeti ya Global.
GPL