ZILIPENDWA wa msanii wa muziki wa kizazi
kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’, amefunguka
kuwa hataki kumsikia mpenzi wake huyo wa zamani kwa madai kuwa amefungua
ukurasa mpya wa uhusiano na mtu ambaye hata hivyo hakuwa tayari kumweka
wazi.
Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Penny alisema hayo hivi karibuni jijini
Dar wakati akizungumza na gazeti hili lililotaka kujua anazungumziaje
tuzo saba za Kilimanjaro alizojizolea Diamond ambapo majibu
yaliyopatikana yalikuwa: “Wanaotakiwa kuzungumzia hili ni mkewe na ndugu
zake, mimi sitaki.”
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Alipoulizwa mke wa Diamond ni nani
alisema: “Mnamjua” na kuicha historia ikibaki kuwa Penny na msanii huyo
waliwahi kuwa katika mapenzi mazito ya njiwa kabla ya kumwagana na
mwanamuziki huyo kumrudia mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu, ambaye
mwenyewe anapenda aitwe mke mtarajiwa. Hahahaha!