Mtuhumiwa Mtonga Omari akitoka mahakamani huku
mikono
ikiwa kichwani akijutia Unyama anayodaiwa kumfanya mtoto huyo wa
marehemu shemeji yake aliyefahamika kwa jina la Mwasiti Said.
Watuhumiwa wa
mtoto anayedaiwa kufichwa kwenye boksi, wamefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi mjini Morogoro, kujibu mashtaka ya kula njama na kufanya
ukatili dhidi ya mtoto huyo.watuhumiwa
hao waliofikisha mahakamani hapo chini ya Ulinzi mkali ni Rashid Mvungi
(47), washtakiwa wengine katika kesi hiyo iliyovutia umati wa watu wa
mji wa Morogoro ni mama mlezi wa Nasrah, Mariamu Said (38) na mume wake
Mtonga Omar (30).
Baba
mzazi wa Nasra Bw Mvungi aliyevaa shati la karoakiingia kwenye mahabusu
ya mahakama ya mkoa akisubiri kupelekwa gerezani baada ya kushinda
kutimiza masharti ya dhamana,Wananchi waliokuwepo mahakamani hapo
walifurahia watuhumiwa hao kupelekwa magereza baada ya kushindwa
kutimiza masharti ya dhamana.
Hatimaye wale
Washtakiwa
hao walifikishwa katika mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi Mary Moyo, Jumatatu ya wiki hii na kusomewa mashtaka hayo.
Wakili
wa Serikali, Sunday Hyera alidai kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo
kati ya Desemba mwaka 2010 na Mei mwaka huu katika mtaa wa Azimio kata
ya Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro.
Wakili
huyo alidai kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa wakiwa walezi wa
mtoto Nasrah, walimfanyia ukatili wa mtelekeza na kumpa malezi akiwa
ndani ya boksi na hivyo kumsababishia magonjwa.
Wakili
huyo wa Serikali, aliyataja maradhi yaliyokumba mtoto huyo akiwa ndani
ya boksi kuwa ni pamoja na utapiamlo, maumivu ya kifua na mvunjiko wa
mifupa katika mwili wake.
Hyera alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kutaja tarehe ya kuisikiliza.
Hata hivyo Wakili huyo aliiomba mahakama kuwa upande wa Jamhuri hauna kipingamizi kuhusu dhamana kwa washtakiwa.
Mahakama
chini ya hakimu wake Moyo, ilisema dhamana kwa washtakiwa iko wazi
lakini kwa masharti ya kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili
watakaosaini bondi ya Sh5 milioni kila mmoja.
Alisema sharti lingine ni wadhamini kuwa na barua kutoka kwa waajiri wa kuaminika au serikali za mitaa.
Hata hivyo washtakiwa walishindwa kutimiza masharti hayo, hatua iliyowafanya warejeshwa gerezani
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 9 mwaka huu itakapotajwa tena..