KIJANA mmoja
wa kiume aliyedaiwa kuwa ni mfanyabiashara ndogondogo amekutwa
amefariki katika kituo cha mabasi yaendayo kasi Manzese, jijini Dar, leo
asubuhi. Inasemekana vijana wengi huwa wana tabia ya kulala ndani ya
vituo hivyo kwa hiyo watu iliwachukua muda mrefu kubaini kama amefariki.
Kwa
mujibu wa mtendaji wa serikali wa Kata ya Midizini-Manzese, Penford
Kizo na mashuhuda wengine, kifo cha kijana huyo hakijafahamika
kimesababishwa na nini.