MAKUBWA! RB nambari TBT/RB/3478/2014 ya Kituo cha Polisi Tabata, jijini Dar es Salaam ina kesi ya dereva taksi aliyepatikana kwa jina moja la Lindoya akidaiwa kuharibu mali za Asia Hakika kwa sababu eti alinyimwa unyumba, Uwazi linakuhabarisha.
Mlalamikaji Asia, mkazi wa Tabata –
Chama na mtuhumiwa Lindoya mwenye makazi yake Mbezi – Makabe ni wapenzi
wa muda mrefu sasa, lakini baada ya Asia kugundua kuwa mwenzake ana mke
na watoto, akagoma kumpa tendo la ndoa, jambo lililoibua kisanga hicho.
Akizungumza na Uwazi, Asia alisema:
“Lindoya ni mpenzi wangu, tulikuwa tunaelekea kuwa mume na mke, maana
tumeishi kwa miaka miwili sasa, lakini siku zote amenieleza kuwa hana
mke wala watoto, lakini nimegundua kuwa alinidanganya.
Asia Hakika akiangalia mali zake zilizoharibiwa.
“Ana mke na watoto wawili, nikaamua
nimuache aendelee na familia yake. Akakataa, anataka kunitumia tu.
Nilipomkatalia ndiyo akaamua kuniharibia vitu vyangu. Alinikuta nina
vitu vya ndani nilivyonunua kwa fedha zangu, nimepanga chumba kwa pesa
yangu na aliniomba tuishi pamoja nikamkubalia.
“Baadaye akaanza kujenga nyumba huko
Mbezi ya Makabe, nilifurahi sana niliamini kuwa tukioana tutakua
tunaishi huko lakini cha kushangaza baada ya kumaliza kujenga alimfuata
mkewe huko Mbeya, wakahamia na watoto wake.”
Alisema, mpenzi wake huyo zilipendwa,
alimwambia asikanyage nyumbani kwake kwa kuwa mkewe amekuja, jambo
ambalo alikubaliana nalo kwa sharti kuwa wasitishe uhusiano wao lakini
Lindoya akaonekana kutoridhika.
Baadhi ya mali za Asia Hakika zilizoharibiwa.
“Siku moja nikiwa kazini, alifika
nyumbani kwangu akafungua mlango kwa funguo wake, maana kila mmoja
alikuwa na wake; akaharibu mali zote ndani, akaacha kitanda tu. Nimeumia
sana kwa kweli,” alisema Asia.
Kwa sasa kesi hiyo ipo katika Kituo
cha Polisi Tabata kwa uchunguzi ambapo jalada la uchunguzi
limeandikishwa kwa namba TBT/IR/2032/2014.
GPL