TAZAMA PICHA::: MWILI WA SISTA ALIYEPIGWA RISASI ENEO LA UBUNGO WAAGWA KWA MAJONZI

Mwakilishi wa mama watawa wakuu wa shirika la malkia kutoka Mbeya akilia kwa uchungu.

SISTA Cresensia Kapuli aliyepigwa risasi Jumatatu Juni 23, 2014 maeneo ya Ubungo, River Side na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi hatimaye ameagwa katika Parokia ya Makoka, Kibangu jijini Dar.

 Masista wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Sista Cresensia Kapuli aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi Juni 23, 2014.
 Mwili wa marehemu umeagwa na umati wa watu wa rika zote wakiwemo viongozi wa dini na serikali. Baada ya kuagwa, mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda jijini Mbeya kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Juni 28, 2014.


 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond H. Mushi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick.
 Sista Brigitte Mbaga aliyekuwa na marehemu Cresensia Kapuli eneo la tukio siku alipopigwa risasi akiwa na simanzi.


 Jeneza likiwekwa ndani ya gari tayari kwa safari ya Mbeya kwa maziko


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...