Timu
ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokjrasia ya Kongo, Mazembe
wameanza vizuri mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuongoza kundi
A, wakiwa na alama sita.
Mchezaji kutoka Zambia Rainford Kallaba alifunga goli pekee lililoipa ushindi TP Mazembe. Kwa matokeo hayo ya Lubumbashi yanamaanisha kwamba Mazembe wanaongoza kundi A kwa alama sita.
Wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, AS Vita Club wako nafasi ya pili, wakipitwa kwa alama mbili.
AS Vita walitoka sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Sudan Al Hilal siku ya Ijumaa.
Kwa upande wa kundi B, Entente Setif ya Algeria walibanwa mbavu kwa sare 1-1 nyumbani kwao na Al Ahli Benghazi ya nchini Libya.