Kujifunga: Eden Hazar amesisiza kuwa na furaha kubakia Chelsea na kumaliza tetezi za uhamisho majira ya kiangazi.
Imechapishwa Juni 10, 2014, saa 5:46 asubuhi
Eden Hazard amedai kuwa kwa `asilimia 100` atabakia Chelsea na amethibitisha kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya.
Eden Hazard amedai kuwa kwa `asilimia 100` atabakia Chelsea na amethibitisha kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya.
Kocha
wa Paris Saint Germain, Laurent Blanc alisema hadharani kuwa klabu hiyo
ya Ufaransa inatamani kumsajili mshambuliaji huyo.
Lakini
mtandao wa Sportmail alhamisi iliyopita ulitoa taarifa kuwa mchezaji
huyo wa kimataifa wa Ubelgiji yuko katika harakati za kusaini mkataba
mpya wa miaka mitano katika klabu yake ya Chelsea na atakuwa analipwa
paundi laki mbili kwa wiki.
Hazard kwasasa anajiandaa kuiwakilisha Ubelgiji kwenye fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
'Nibakia Chelsea, nina asilimia 100`, alisema nyota huyo mwenye miaka 23.
`Kiukweli katika mpira huwezi kujua, lakini nipo chini ya mkataba na Chelsea na nataka kukaa pale`.
"Nipo katika mazungumzo ya mkataba mpya na Chelsea. Mazungumzo ndio kwanza yanaanza, lakini bado tuna muda".
"Lakini
ukweli ni kwamba, Chelsea wamenipa ofa ya mkataba mpya ambao utanifanya
nijiamini zaidi, kwamba nitafanya kazi nzuri zaidi na watanifurahia".
Hazard yuko mbioni kuanza kula mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki katika mkataba mpya na Chelsea
Laurent Blanc anataka kumsajili Hazard katika klabu yake ya Paris Saint-Germain majira ya kiangazi.