Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Juni 10, 2014, saa 10:30 asubuhi
KAMATI
ya rufani ya shirikisho la kandanda Tanzania, TFF chini ya mwenyekiti
wake, mwanasheria Julius Lugaziya leo mchana inaendelea kumalizia
kujadili rufani ya mgombea aliyeenguliwa kuwania nafasi ya urais katika
uchaguzi wa Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu, Michael
Richard Wambura.
Kikao
cha kamati hiyo kilianza jana majira ya saa 5:00 asubuhi katika hoteli
ya Courtyard, Upanga, jijini Dar es salam na kuahirishwa saa 4:30
usiku, lakini ngoma ililala bila kufikia maamuzi na leo hii kamati
inatarajia kukutana tena saa 6:00 mchana ili kumalizia na kufikia
maamuzi ya mwisho.
Hamu
ya wadau wengi wa soka na wanachama wa Simba wanahitaji kufahamu kama
Wambura anarudishwa au anaondolewa rasmi katika kinyang`anyiro hicho.
Jana
kamati ya Lugaziya alifikia sehemu nzuri kwa kuhoji pande zote mbili
kwa maana ya wakata rufaa na wakatiwa rufaa na leo wanaanza kupitia
maelezo yao na kuyapima uzito na kufanya maamuzi.
Mtandao
huu umekuwa ukipokea simu na jumbe fupi za simu kutoka kwa wadau wake
wakiuliza nini maamuzi ya kamati ya rufani ya TFF iliyokutana jana.
Jana
timu yetu ilipiga kambi maeneo ya Courtyard kufuatilia `ngado kwa
ngado` kinachoendelea kwenye kamati hiyo ili kuja na jibu sahihi, lakini
kulikuwa na usiri mkubwa mno, japokuwa kila mtu alikuwa anasema lake.
Hata siku moja, mtandao huu hauandiki taarifa ambayo haijathibitishwa na vyonzo makini.
Ukipita kwenye mitandao ya kijamii, watu wengi wanaandika kuwa Wambura karudishwa wengine wanasema kaondolewa.
Taarifa hizi si rasmi kwasababu maamuzi hayajafikiwa mpaka sasa.
Kuna uwezekano hatima ya Wambura ikajulikana leo jioni, kwahiyo wadau wetu kuweni na subira.
Taarifa
za kwenye mitandao si za kiziamini kwa asilimia zote kwasababu kuna
uhuru wa kuandika na kuchapisha habari. Wengine wapo kwa ajili ya
kuwavutia wasomaji, lakini sisi hatufanyi kazi kwa misingi hiyo.
Hatujapata taarifa rasmi na wahusika walisema wanakaa tena leo, kwa maana hiyo taarifa rasmi itatoka leo.
Asante kwa kuwa nasi na tutazidi kuwafahamisheni kinachoendelea kwa wakati huu.