NEYMAR AITETEMESHA BRAZIL NZIMA, LAKINI MAMBO YAWA SHWARI KABISA....

Anguish: Neymar looks in real pain as he goes down clutching at his right ankle




Imechapishwa Juni 10, 2014, saa 5:26 asubuhi.

BRAZIL nzima jana ilizizima baada ya nyota wake kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika mazoezi na hofu kubwa kundanda juu ya ushiriki wake katika fainali za kombe la dunia.
 Nyota huyo wa Barcelona aliteguka kifundo cha mguu wakati Selecao wakifanya mazoezi nje ya Rio Janeiro na kumlazimu kupata matibabu ndani ya uwanja.
Hata hivyo baada kukaa chini kwa dakika kadhaa, nyota huyo tegemeo kwa kombe la dunia aliweza kusimama mwenyewe na kutembea bila tatizo lolote.
Nervy moment: Neymar (far left) rolls his right ankle while running in Brazil's evening training session
Neymar (kwa mbali kushoto) aliteguka kifundo cha mguu wakati akikimbia katika mazoezi.
Neymar alirudi uwanjani mapema na kuonekana kuwa fiti kuanza katika mechi ya ufungzi dhidi ya Croatia alhamisi ya wiki hii.
Wakati huo huo, Brazil, inafanya kazi ya kuboresha safu yake ya ulinzi kuelekea mchezo wa ufunguzi.
Kocha Luiz Felipe Sccorali alitumia muda mwingi katika mazoezi ya jumatatu kufanya maboresho ya beki yake na aliwabadilisha badilisha wachezaji ili kuwa na ukuta imara.
Ingawa Brazil hawakufungwa bao lolote katika mechi zao za majaribio, Scorali alisema safu yake sio nzuri, hivyo ni muhimu kulifanyia kazi haraka.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...