Mgeni
rasmi Jesca Msambatavangu mwenye kashda ya Tanzania shingoni akiwa na
baadhi wa wavunaji wa asali kabla ya kwenda kuvuna asali na baadaye
katika hafla ya kukabidhiana mashine za kukamua asali na mizinga ya
nyuki pamoja na mavazi maalum ya uvunaji asali iliyofanyika katika
kijiji cha Kinywang’anga hivi karibuni.
Mgeni
rasmi Jesca Msambatavangu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa
akikabidhi mmoja wa wenyeviti wa vikundi mashine ya kukamua asali hafla ya kukabidhiana mashine za kukamua asali na mizinga ya nyuki pamoja na mavazi maalum ya uvunaji asali.Afisa misitu mstaafu Teresphory Kahatano akitoa maelekezo kwa walinaji wa asali kabla ya kwenda katika mizinga ya nyuki.Baadhi ya mashine za kukamua asali na mavazi rasmi yaliyokabidhiwa kwa vikundi 6 vya ujasiliamali.Mgeni
rasmi Jesca Msambatavangu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa
akikabidhi mmoja wa wenyeviti wa vikundi moja ya mizinga iliyotolewa na
TaFF kwa kushirikiana na MJIMUKK. (Picha zote na Denis Mlowe)
…………………………………………………………………………………………..
Na Denis Mlowe,Ismani
MFUKO
wa Hifadhi ya Misitu Tanzania (TaFF) kwa kushirikiana na Mtandao wa
Jamii wa Usimamizi wa Misitu Kanda ya Kitapilimwa (MJUMIKK) umewakabidhi
mashine sita za kukamua asali na mizinga ishirini kwa vikundi vya
ujasiriamali vinavyojishughulisha na ulinaji wa asali katika kata za
Kitapilimwa na Kiwele katika jimbo la Ismani mkoani Iringa
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika kijiji cha Kinywang’anga hivi karibuni, katibu wa mtandano wa MJUMIKK, Samson Fuko alisema lengo la msaada huo ni kuleta ufanisi wa kulinda, kutunza na kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na kuongeza kipato cha mwananchi mjasiriamali.
Alisema mashine hizo zitakuwa shamba darasa la ufugaji wa nyuki na upandaji miti utakaotumika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanachama wake na kutoa elimu kwa jamii juu ya uhifadhi wa mazingira.
Fuko alisema mtandao huo umefanikiwa kuongeza idadi ya wanachama kutoka 50 waliokuwa mwanzao hadi wanachama 200 walioko sasa ambao unajihusisha na ufugaji wa nyuki unaotekelezwa katika vijiji sita kati ya vijiji 11.
Alivitaja vikundi vilifaidika na msaada huo kuwa ni Kinywang’anga, Faraja group, Twiga group, Mshikamano. Jitegemee na kikundi cha Umoja vyote vikipatiwa mizinga mashine na za kukamulia asali pamoja na mavazi maalumu ya kuvaa wakati wa kulina asali vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 4.5
Aidha aliwataka wadau kuvisaidia vikundi vya ufugaji nyuki mizinga ya nyuki na mbegu za miti kwa lengo la kuanzisha shamba darasa la ufugaji wa nyuki na shamba darasa la upandaji miti na mavazi ya kuvunia asali kwa vikundi hivyo.
Kwa upande wake mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu aliyekuwa mgeni rasmi katika makabidhiano ya mashine hizo amewaasa wazazi na walezi kuwahamasisha vijana kujiunga katika shughuli za maendeleo wasiwaache wakilegalega kwani vijana hao ndio nguvu kazi ya taifa
Alisema maendeleo ya mtu hayaletwi kwa kukaa bila kujishughulisha na kukaa vijiweni na kuwataka wajasiliamali hao kutumia fursa waliyoipata kuitumia katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Aidha Msambatavangu aliwahidi wafugaji nyuki kuwatafutia soko la bidhaa zao kuweza kuwafikia watu wengi zaidi katika jamii ya mkoa wa Iringa na nje ya nchi.
Msambataangu ambae pia ni mlezi wa vikundi hvyo amewaeleza wananchi kuwa kiongozi bora ni yule anaetekeleza majukumu aliyopewa na wananchi na sio kuwadharau wale waliompa dhamana ya kuwa kiongozi
Msambatavangu amewataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kuwatumikia na kuwatatulia matatizo yao mda wowote wanapowahitaji na kuwajibika sio kukaa na kutoa lawama

Aidha
amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa
Pudensiana Kisaka kwa kazi anayofanya ikiwa ni moja ya utekelezaji
wa majukukumu aliyopewa na serikali na amesema kuwa kiongozi huyo
anapaswa kuigwa na viongozi wa halimashauri nyingine kwani amekuwa
akisikiliza matatizo ya wananchi katika halimashauri yake na
kuyafanyia kazi.