KARIA KUFUNGUA KOZI YA MAKOCHA LEO
Makamu wa Raiswa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia atakuwa
mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kocha ya makocha wa mpira wa miguu ya
Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Uzinduzi
wa kozi hiyo ya wiki mbili utafanywa leo (Juni 10 mwaka huu) saa 6
mchana kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam.
Makocha
zaidi ya 20 wenye Leseni C kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki
katika kozi hiyo inayoendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni.
Mkufunzi mwingine wa kozi hiyo anayetambuliwa na CAF ni Mkurugenzi wa
Ufundi wa TFF, Salum Madadi.
KANALI MWANAKATWE KUZIKWA LEO BABATI
Maziko
ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
wakati huo likiitwa FAT, Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe
yanafanyika leo (Juni 10 mwaka huu) Magugu, Babati mkoani Manyara.
Kanali
Mwanakatwe alifariki dunia Juni 7 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya
Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu baada
ya kuanguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach.
TFF
imetoa ubani wa sh. laki tano kwa familia ya marehemu Kanali
Mwanakatwe, na katika maziko hayo inawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji wa Kanda ya Arusha na Manyara, Omari Walii.
AMBUNDO, SHIZA WATESA UHOLANZI
Wachezaji wa Tanzania walioko Uholanzi, Dickson Ambundo na Shiza Yahya wameanza kuonekana muda na waandaaji wa mashindano ya AEGON Copa Amsterdam.
Kwa
mujibu wa wakala wa wachezaji wa Uholanzi, Denis Kadito, AEGON Copa
Amsterdam ni mashindano ya kimataifa yanayoshirikisha timu kubwa kutoka
nchi mbalimbali ulimwenguni kwa wachezaji wa miaka chini ya 19.
Kwa
Uholanzi, Ajax Amsterdam huwa lazima washiriki, na pia huwa kuna timu
ya ridhaa inayotengenezwa kwa kuchagua “best talent” kutoka Uholanzi.
Mchujo wa wachezaji hao kutengeneza timu ya kombaini, ulianza na
wachezaji wasiopungua 1,000.
Kombaini
hiyo inaitwa Men United na inafundishwa na mchezaji wa zamani wa
kimataifa wa Uholanzi, Ronald de Boer. Ronald e Boer ni pacha wa kocha
wa Ajax (First team).
Ronald
de Boer pia ni kocha wa wachezaji washambuliaji wa Ajax. Shiza na
Ambundo waliingizwa kwenye mchujo na wakafanya vizuri, mwishoni wakaitwa
kwenye timu ya wachezaji 18 waliotengeneza timu ya Men United. Hii ni
mara ya kwanza wachezaji wasio Waholanzi kuingizwa katika timu hiyo.
Mashindano
ya Copa Amsterdam yameanza juzi (Juni 8 mwaka huu) na yanaisha kesho
(Juni 11 mwaka huu. Katika mashindano hayo kuna makundi mawili. Kundi A
ni AFC Ajax (Amsterdam), Ajax Cape Town ( Afrika Kusini), Fluminense
(Brazil), Hamburg SV (Ujerumani) wakati B ni Men United, Panathinaikos
(Ugiriki), FC Aerbin (China) na Cruizero (Brazil).
Shiza
na Ambundo wamecheza mechi zote tatu. Shiza amekuwa akicheza namba tatu
wakati Ambundo anapiga namba tisa, saba na kumi na moja.