Limeingia? Karim Benzema akianza kushangilia akiamini ameifungia Ufaransa bao la pili dhidi ya Honduras.
TEKNLOJIA
ya Goal Line hatimaye imetumika usiku huu kwenye mechi ya kombe la
dunia. Karim Benzema amefunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi
ya Honduras, mchezo wa kombe la dunia wa Kundi E mjini Porto Alegre.
Mshambuliaji
huyo wa Real Madrid aliifungia Ufaransa bao la kuongoza kwa mkwaju wa
penati iliyotokana na Wilson Palacios kumfanyia madhambi katika eneo la
hatari, Paul Pogba na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Benzema alifanya kazi kubwa katika bao la pili, lakini bao hilo alipewa kipa wa Honduras, Noel Valladeres, kuwa amejifunfa.
Benzema allifunga bao tatu kwa shuti kali na kukamilisha karamu ya mabao 3-0.
Utata:Teknolojia ya kwanza ya Goal line ilionesha hakuna goli, lakini iliangaliwa upande ambao si sahihi .
Imethibitisha: Lakini mara ya pili ilionesha kuwa mpira ulivuka mstari.
Noel Valladares akijaribu kuzuia mpira usiingie nyavuni, lakini kaishia kujifunga.
Acha zakeo refa!: Wachezaji wa Honduras walikuwa na uhakika kuwa siyo goli.
Karim Benzema akiifungia Ufaransa bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati.
Mlinda mlango akiambulia manyoya
Wilson Palacios alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuchezea vibaya Paul Pogba.