KUMBUKUMBU YA MIAKA SABA TANGU KIFO CHA BABA YETU MPENDWA:. LAURENCE LUCIAN MBALAHAMI

Marehemu Laurence Lucian Mbalahami
  Baba yetu Mpendwa, leo umetimiza miaka saba (7) tangu ulipoitwa ghafla na Mwenyezi Mungu aliye juu Mbinguni na mkuu na muweza wa yote duniani na mbinguni mnamo terehe 21 July 2007.  
 
Tunakukumbuka kwa mengi sana hasa malezi bora kwetu, elimu, ushauri, ucha Mungu na mengine mengi.

Kila mmoja wetu, kwa namna ya kipekee, anakumbuka upendo wako wa dhati kwetu sisi wote, wanao na wakwe zako bila ya ubaguzi wowote. Upendo wako kwetu umekuwa nuru na mfano wa kuigwa nasi na umetufanya tushikamane na kupendana sana na tunamuomba Mwenyezi Mungu ili tudumu kwenye mshikamano na upendo huo.

Unakumbukwa sana na wanao wapendwa Walter, Ciliel, Anna, Laurence na Josephine, wadogo zako Hortencia Mbalahami,
Lucy Mbalahami, Leonce Mbalahami, Fortnatus Mbalahami, Mussa Mbalahami na Enock Mbalahami.

 Wajukuu zako Beatrice na Louis pamoja na  ndugu, jamaa na marafiki.

RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWAANGAZIE.
APUMZIKE KWA AMANI, AMINA.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...