NI ZAIDI YA SODOMA: MACHANGUDOA ZAIDI YA 20 WAKAMATWA WAKIWA WANAJIUZA

BAADHI ya akinadada wanaofanya biashara haramu ya kujiuza katika maeneo ya Jiji la Dar, wameeleza kuwa licha ya kupewa kashikashi na jeshi la polisi na wakati mwingine kukamatwa na kupelekwa mahakamani, hawawezi kuiacha ‘kazi’ hiyo kutokana na ugumu wa maisha.
Wadada hao waliyasema hayo, juzi Jumatano baada ya kunaswa na paparazi wetu maeneo ya Sinza Afrikasana pembeni ya Corner Bar ikiwa ni siku  chache baada ya baadhi yao kukamatwa na polisi ambapo walisema biashara hiyo ndiyo maisha yao.
Walisema, hawapendi kuifanya lakini wanalazimika kutokana na maisha duni waliyonayo.
“Nani asiyependa kulala usiku na familia yake? Ukituona barabarani ujue hali ni mbaya. Hata kama polisi wanatukamata lakini wanatuachia na tunarudi sokoni kama kawaida,” alisema changu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Zuena na kuongeza:
“Wateja wetu wenyewe wanajua kuwa hii nguvu ya polisi ni ya soda tu, wakiona tumepigwa ambushi kidogo wanasubiri zipite siku chache kisha tunaendeleza harakati zetu, sisi bila kuja kujiuza hatuwezi kuwasomesha watoto wetu wala kuwalisha.”
Katika hali ya kushangaza wakati changudoa huyo akizungumza hayo, wapo waliokuwa wakimshawishi paparazi wetu anunue ngono kwa maelezo kuwa, hali ni mbaya kwani polisi wamekuwa wakifanya doria mara kwa mara.
“Sasa, achana na mambo ya kutuhoji bwana, tutoe basi kama vipi tukuuzie mambo kwa bei ya ofa. Cheki nilivyojaaliwa,” alisema binti mmoja ambaye ukikutana naye mchana unaweza kusema, ‘mke si ndiyo huyu’.
Hata hivyo, katika pitapita ya mwandishi wetu maeneo mengi kama vile Kinondoni, Sinza Mapambano, Mwenge Bamaga na Buguruni, madadapoa hao wameonekana wakiendelea kujiuza kwa kuibia huku wakiwa makini na kila mteja anayewatokea.
Aidha, gazeti hili linalipongeza Jeshi la Polisi jijini Dar kwa operesheni ambazo limekuwa likizifanya kwani kwa namna moja ama nyingine kasi ya biashara hiyo imepungua licha ya kwamba
wanatakiwa kuongeza nguvu zaidi. Pia taasisi za ustawi wa jamii na serikali kwa jumla zinatakiwa kuangalia mbinu mbadala za kuweza kuwaondoa akinadada hao kwenye mazingira hayo hatarishi.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...