Mwili wa aliyekuwa msanii wa filamu Bongo, Patrick August, ‘Bryton’ ukiwa ndani ya gari.
TASNIA ya
filamu Bongo imepata pigo tena baada ya msanii aliyekuwa akichipukia
kwa kasi, Patrick August ‘Bryton’ kufariki dunia kwa ajali mbaya ya
pikipiki.Akizungumza na paparazi wetu, Mwenyekiti wa Sherehe na Maafa
kwa wasanii wa Wilaya ya Kinondoni, Masoud Kaftany alisema Bryton
alipata ajali usiku wa kuamkia Jumapili maeneo ya Tabata - Relini wakati
akirejea kwao maeneo ya Tabata - Kinyerezi.“Alikuwa
akiendesha mwenyewe pikipiki, akavaana uso kwa uso na gari, ilikuwa ni
ajali mbaya sana kwani marehemu alipasuka vibaya kichwa hali
iliyosababisha damu nyingi kuvuja na kusababisha kifo chake,” alisema
Kaftany.
Marehemu Patrick August, ‘Bryton’ enzi za uhai wake.
Baadhi ya
sinema alizoigiza enzi za uhai wake ni pamoja na Muuza Genge na Mapenzi
ya Fukara iliyomshirikisha Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wasanii wengine.
Mwili wa
marehemu Bryton ulisafirishwa jana (Jumanne) kwenda Rombo, mkoani
Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyikwa leo Jumatano.SHUKRANI KWA GPL