THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi kufuatia ajali iliyotokea tarehe 30 Julai,
2014 katika eneo la Pandambili, Wilayani Kongwa na kuua watu wapatao 18.
Katika
ajali hiyo, watu 13 walifariki katika eneo la ajali, na majeruhi
wapatao 56 walifikishwa hospitalini. Kati ya majeruhi hao hadi sasa
waliolazwa ni 30 na wengine wameruhusiwa baada ya kupata matibabu.
Rais
amemuomba Dkt. Nchimbi kumfikishia rambirambi zake za dhati kwa ndugu
na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo, na kuwapa pole
majeruhi wote na kuwatakia kupona haraka ili warejee kwenye shughuli zao
za kila siku.
“
Natoa Pole za dhati kwa wale wote walioondokewa na wapendwa wao katika
ajali hii na pia kuchukua nafasi hii kuwapa pole majeruhi wote na
kuwaombea kupona haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku”. Rais amesema katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
“Hakika
ni jambo la kusikitisha sana kuondokewa na wananchi wetu katika ajali ,
natoa wito wangu kwa madereva wote na wote wanaotumia vyombo vya moto
kuwa makini wanapokuwa barabarani “. Rais amesema na kuongeza kuwa;
“Kila
dereva anaetumia chombo cha moto, ana wajibu wa kulinda maisha yake na
ya watumiaji wengine kwa kuwa makini na muangalifu awapo barabarani,
kwani ajali hizi zinarudisha nyuma maendeleo ya taifa na ya wananchi kwa
ujumla” Rais amesema na kuvitaka vyombo vya
ulinzi na usalama barabarani kutolegeza kamba katika kuwachukulia hatua
madereva wasio makini na wazembe wakati wote”.Rais amesisitiza.
Taarifa
kutoka Mkoani Dodoma zinasema ajali hiyo ya jana (30 Julai, 2014)
ilisababishwa na Lori ambalo lilitaka kupita lori jingine na hivyo
kwenda kugongana uso kwa uso na Basi la Moro Best lililokuwa likitokea
Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.
……Mwisho……
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
30 Julai, 2014