TIMBWILI! Jamaa mmoja na mkewe ambao wote hawakujulikana
majina mara moja wamezua varangati la aina yake mahakamani kisa kikiwa ni
kufutiwa kesi na kushindwa kuheshimu amri za maafande.Tukio hilo la aina yake
lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar baada ya mume huyo kufutiwa kesi iliyokuwa
ikimkabili ya
unyayasaji wa watoto wake wa kuwazaa. Jamaa huyo na mkewe walizua timbwili hilo
wakati mtuhumiwa huyo akitolewa chumba cha mahakama kwenda kuweka sawa nyaraka
ili awe huru.
Huku akiwa na hasira, mwanaume huyo alianza kuzozana na
polisi huku akiungwa mkono na mkewe wakikataa kutii amri ya askari aliyekuwa
akiwaelekeza kwenda chumba kingine ili kukamilisha taratibu za kuwa huru.
Akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Wawili hao walisikika wakitoa maneno makali kuwa wasisukumwe
kwani hakimu alikuwa ameshamwachia mwanaume huyo huru, jambo ambalo liliwakera
askari na kuwaambia kuwa wanatakiwa kutii sheria na taratibu za mahakama.
Katika sekeseke hilo huku askari wakilazimika kutumia nguvu,
jamaa huyo alifanya mgomo baridi akipiga kelele na kufoka hivyo kusababisha
watu kushangaa.
Hata hivyo, polisi hao walitumia mbinu ya kuwadhibiti
kistaarabu ili kuhakikisha amani inakuwepo mahakamani hapo hivyo mambo yakawa
shwari.
Mwanamke huyo akidhibitiwa.
Habari ndani ya
mahakama hiyo zilidai kwamba jamaa huyo alikuwa akikabiliwa na tuhuma hiyo ya
unyanyasaji wa watoto wake ambao alizaa na mwanamke mwingine. Madai yalishushwa
kwamba mwanaume huyo alikuwa akishirikiana na mkewe huyo mpya kuwafanyia
manyanyaso kwa watoto wake hali ambayo iliyosababisha shirika moja la kutetea
haki za binadamu kumchukulia hatua ikiwa
ni pamoja na kumfikisha mahakamani hapo.
Ilisemekana
kwamba jamaa huyo alionywa na kupewa maelekezo kuwa kama ikiwezekana
watoto hao watafutiwe sehemu nyingine ya kuishi ikiwa ni
pamoja na kupata mahitaji muhimu, jambo ambalo mwanaume huyo
alilitekeleza na
kumaliza ishu hiyo.