MSANII na prodyuza wa Bongo Fleva na Ragga, Mack Malik Simba ‘Mack 2B’ amefariki dunia. Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Msafiri Masharubu, Mack 2B amekutwa na umauti leo asubuhi akiwa nyumbani kwao Yombo, jijini Dar es Salaam. Masharubu alieleza kuwa Mac alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba miguu. Enzi za uhai wake, marehemu alikuwa memba wa Kundi la Wateule na prodyuza kwenye studio za Enrico pale Sound Crafters.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!