Home »
Uncategories »
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA WAKATI WA VURUGU ZA MBAGALA LEO
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA WAKATI WA VURUGU ZA MBAGALA LEO
Unknown
6:29 PM
Askari kanzu katika jitihada za kuwatawanya waandamanaji.
Mojawapo ya matairi yaliyochomwa na wananchi.
Waananchi wakiandamana wakati wa vurugu hizo.
Askari polisi wakiwa eneo la tukio.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert Kiondo (wa tatu kulia) akiwa katika eneo la tukio.
Kamanda Engelbert
Kiondo (wa pili kulia) akipokea maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wa
serikali ya mtaa wa Kizuiani, Mashaka Selemani (wa kwanza kushoto).
Kamanda Kiondo akitoa maelekezo kwa baadhi ya askari wake.
Wananchi wakiwa eneo alipogongwa mwanafunzi.
Kikosi cha polisi jamii kikiwa eneo hilo.
OCD wa Mbagala, Jonathan Shanna akiwasiliana na kikosi chake.
LEO asubuhi majira ya saa nne na nusu kumetokea vurugu kali za wananchi eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.
Vurugu hizo zilitokea baada ya mwanafunzi mmoja kupoteza maisha kwa
kugongwa na lori lenye namba za usajili T 632 BVY. Baada ya ajali hiyo,
wananchi walifunga barabara kwa mawe na kuchoma matairi wakizuia magari
kupita katika barabara ya Kilwa jambo lililopelekea polisi kuingilia
kati. Ili kutuliza vurugu hizo kutoka kwa wananchi waliokuwa wanadai
kuchoshwa na ajali zinazotokea mara kwa mara eneo hilo, polidi
walilazimika kutumia mabomu ya machozi pamoja na kupiga risasi hewani
katika kuwatawanya wananchi.
(Picha na Makongoro Oging’ / GLP)