KATIBU MKUU KIONGOZI WA UINGEREZA AWASILI NCHINI TANZANIA KWA ZIARA


Picture
Sir Simon Fraser
Picture

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Alhamisi Oktoba 3, 2013
Ziara ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Uingereza na Mkuu wa Diplomasia katika ofisi ya mambo ya nje na Jumuiya ya Madola 
Katibu Mkuu kiongozi wa Uingereza na mkuu wadiplomasia katika ofisi ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola, Sir Simon Fraser, amewasili nchini Tanzania asubuhi hii kama sehemu ya ziara yake ya kanda; Tanzania, Sudan na Sudan ya Kusini.
Ziara hii inatoa taswira ya umuhimu wa kihistoria na kimkakati unaoendelea baina ya Tanzania na Uingereza na kudhihirisha mahusiano bora yaliyopo. Uingereza tayari ni mwekezaji mkubwa nchini Tanzania na ni mfadhili mkubwa wa pili. Kwa mwaka
huu pekee, Idara ya Maendeleon ya Kimataifa ya Uingereza yenye kuratibu shughuli za maendeleeo (DFID) itatumia Paundi Milioni 150 (sawa na TZS 390 Bilioni) katika shughuli za maendeleo nchini Tanzania.

Ziara ya Sir Simon inafuatia mafanikio makubwa ya ziara ya Waziri wa Uingereza mwenye dhamana ya Afrika, Mark Simmonds, mwezi Julai ambapo Rais Kikwete aliafiki mahusiano mapya ya juu kati ya Uingereza na Tanzania katika kusimamia ustawi, mahusiano ambayo yanaongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda yanayotoa fursa zenye kusisimua katika maeneo ya uziduaji (extractive industry), kilimo na sekta ya nishati endelevu vilevile mazingira ya kibiashara kwa upana wake. Matumaini ya Uingereza kupitia ushirikiano wa kibiashara ni kuongeza biashara na uwekezaji na kusaidia maendeleo ya Tanzania na kuzaa ustawi na ajira kwa Tanzania na Uingereza. Hii inaenda sambamba na msaada wa Uingereza kwa serikali ya Tanzania katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.

Akizungumza kabla ya ziara, Sir Simon alisema:

“Uingereza inaiona Tanzania kama moja ya wadau wake muhimu sana Afrika na ninayo fahari kuitembelea kwa mara ya kwanza. Ninatarajia kusikia mwenyewe toka kwa wahusika wenyewe juu ya uwepo wa fursa nyingi nchini Tanzania na kuelewa vyema namna gani Uingereza inaweza kuiongeza tija.

Licha ya kwamba Uingereza tayari inaongoza katika uwekezaji Tanzania, bado tunahitaji kuwekeza zaidi. Tunataka kufanya kazi kwa ushirika kusaidia Tanzania kuweza kufikia malengo ya kuwa taifa la uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kunufaisha wananchi wake wote. Tunataka kufanya haya kwa dhamira ya kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi zetu mbili na kuendelea kuisaidia Tanzania kimaendeleo. Ni matumaini yangu katika zaira yangu italeta matunda katika ushirikiano wetu wa kiuchumi na kutafuta namna ya kusaidia kuboresha mazingira ya kibiashara”

Katika ziara yake, Sir Simon atakutana na Waziri wa Viwanda na Biashara, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji na Uwezeshaji, Viongozi toka Kitengo cha Rais-Utekelezaji (President’s Delivery Bureau), na makampuni kadhaa ya Uingereza,  Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania.

__________________________________________________________

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na; 

Michael Dalali
Afisa Miradi na Habari
Ubalozi wa Uingereza
Dar es Salaam

Simu: +255 (0) 22 229 0269
Simu ya Mkononi: +255 (0)762 791 991


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...