Miguu ya Thom Malenga ikiwa imevimba vibaya baada ya kuteswa
vikali na kikosi cha kupambana na ujangili nchini kwa tuhuma
zisizo na uchunguzi
Mzee Lutumwa ambae alikamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao
wa ujangili japo si kweli na ndio sababu ya leo kuachiwa huru
Bw Thom Malenga akiwa na mmoja kati ya mtuhumiwa wa ujangili
aliyeachiwa leo kati ya watu saba akiwemo Malenga walioachiwa
baada ya kukosekana ukweli wa tuhuma dhidi yao.
KATIBU msaidizi wa mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa Bw Thom Malenga aliyekamatwa kwa tuhuma hewa za kujihusisha na ujangili wa meno ya tembo pamoja na watuhumiwa wengine sita leo wameachiwa baada ya kuhojiwa na kuchunguza tuhuma hizo dhidi yao .
Watuhumiwa hao ambao walikamatwa kwa nyakati tofauti na kikosi maalum cha kupambana na ujangili katika Hifadhi ,kikosi kinachoundwa na askari wa JWTZ , usalama wa Taifa na askari wa kawaida leo wameachiwa baada ya kuteswa vibaya ili kuwataja watu ambao wanadai kuwa wameandikwa katika orodha yao.
Hata hivyo inadaiwa kuwa askari wa JWTZ ndio ambao wamekuwa wakiwatesa kwa kuwapiga watuhumiwa hao huku wakilazimishwa kuwataja watu ambao majina yao yapo na wao wenyewe wahusika wa kikosi hicho.
Malenga alisema si kweli kama alikamatwa na meno ya tembo kama ambavyo gazeti la Rai la jumapili limepata kuripoti na kuwa yeye alikamatwa akiwa ofisini na hadi sasa ameachiwa baada ya kikosi hicho kufanya uchunguzi wake na kuona suala hilo halina ukweli wowote na kama kweli angekuwa anahusika basi asingeachiwa na watu wengine ambao walikuwa wakishikiliwa pamoja na yeye .
Hata hivyo alisema hadi sasa bado kuna watu ambao wanashikiliwa katika kambi hiyo iliyopo eneo la Hifadhi.
Malenga ambae amejeruhiwa vibaya katika mikono yake pamoja na miguu yote miwili anaendelea kupatiwa matibabu na kwa sasa hawezi kutembea kutokana na mateso aliyoyapata.
Mtandao huu utaendelea kukueleza jinsi mateso ambayo watuhumiwa wamekuwa wakiyapata ambapo mzee Andrea Lutumwa (77) mkazi wa Ikanga Mbarali mkoani Mbeya ataanika kila kitu hapa.
Wakati huo huo wanahabari mkoa wa Iringa kesho jumanne watakutana kuzungumzia suala la gazeti la rai jumapili kuandika habari za upotoshaji kuhusu sakata hili kwa kudai kuwa wanahabari mkoa wa Iringa wamehongwa na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa ili wasiandike habari hiyo.

Chanzo; Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::