Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi akiwakaribisha baadhi ya maofisa wa kike kutembelea kiwanda hicho.
Editha Mushi akitoa maelezo kwa baadhi ya maofisa.
Mmoja wa maofisa wa kikosi cha usalama barabarani akijitambulisha.
Mtaalamu
wa Upishi wa Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Calvin Nkya (kulia)
akielezea jinsi bia inavyopikwa kwa njia ya kisasa wakati maofisa wa
kikosi cha polisi cha usalama barabarani, walipotembelea kiwanda cha
kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi kujua utendaji wake. TBL hivi karibuni
ilidhamini maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
yaliyomalizika hivi karibuni.
Mtaalamu
wa Upishi wa Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Calvin Nkya (kulia)
akitoa maelezo kuhusu utendaji wa kiwanda cha bia cha Dar es
Salaam,wakati maofisa wa kikosi cha polisi cha usalama barabarani,
walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. TBL
ilidhamini maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
yaliyomalizika hivi karibuni.
Consolata Adamu wa TBL, akielezea kuhusu kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt.
Nkya akitoa maelezo kuhusu utendaji wa kiwanda cha Bia cha Dar es Salaam.
Maofisa wakitembezwa katika moja ya idara ya utengenezaji bia.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi, Ibrahim Mwamakula (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve
Kilindo, wakati maofisa wa kikosi cha polisi cha usalama barabarani,
walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam kujua utendaji
wake. TBL hivi karibuni ilidhamini maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani yaliyomalizika hivi karibuni.
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Mrakibu wa Polisi, Meloe Buzema akipokea zawadi kutoka kwa Kilindo.
Maofisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TBL, baada ya kumaliza ziara.
PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG