Shaabani Maulidi anayedaiwa kufa na kufufuka akiwa katika hospitali ya wilaya Geita.
Baadhi ya mifupa kutoka katika kaburi analodaiwa kuzikwa Maulid ikichukuliwa kwa uchunguzi.
Na Mwandishi Wetu, Geita
MTOTO Shaabani Maulidi anayedaiwa kufa na kufufuka mkoani Geita miaka mitatu iliyopita baada ya kutumbukia kisimani mwaka 2011 amekuwa gumzo mjini hapa.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia watu wakimiminika hospitali ya Geita alikolazwa mtoto huyo ili kumuona, hali iliyowapa shida wazazi wake.

...Kaburi linalodaiwa kuwa la Maulid likifukuliwa.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita ambapo mtoto huyo alilazwa kwa matibabu, alisema kuwa hali yake inaendelea vizuri na wakati wowote ataruhusiwa.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli juu ya tukio hilo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka hospitali hiyo, ambapo kwa sasa hatua inayoendelea ni kutafuta vipimo vya vinasaba (DNA).

...Wananchi wakiwa ndani ya kaburi ili kuchukua baadhi ya mabaki kwa uchunguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamnda wa Polisi wa Mkoa wa Geita ACP Leonard Paulo, alisema kuwa pamoja na kuthibitisha tukio la kuonekana kwa mtoto huyo akiwa hai bado serikali haiamini kama ni kweli alikufa na kufufuka.
“Mimi kama kamanda wa polisi na serikali kwa ujumla, hatuamini kama mtoto huyu alikufa na kufufuka japo wazazi wake wanakiri kuwa mtoto wao alikufa na sasa amefufuka. Serikali kwa kawaida haiamini mambo kama hayo na ndiyo maana tumeamua kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hili,” alisema Kamanda Paul.