Wanajeshi wawili wa Kenya wafungwa kwa uporaji wakati wa tukio la Westgate

130923105957_kenya_army_512x288_afp
Wanajeshi wawili nchini Kenya wamefukuzwa kazi na kufungwa jela kwa kitendo cha uporaji waliofanya wakati wa shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la Westgate mwezi uliopita. Video za CCTV ziliwaonyesha wanajeshi hao wakitoka na mifuko kutoka kwenye maduka yaliyopo kwenye mall hiyo.
Mkuu wa jeshi Julius Karangi alisema kuwa mwanajeshi wa tatu aliyeshukiwa kwa uporaji bado anachunguzwa. Hapo mwanzoni mkuu huyo wa majeshi alikanusha hizi habari hadi zilipotoka video za CCTV ambapo kwenye tukio hilo walifariki watu 67 na wengine mamia kujeruhiwa.
Wakati huohuo, mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa uhalifu katika idara ya polisi Ndegwa Muhoro alisema kuwa mmoja wa magaidi waliokuwa ndani ya jengo hilo walipiga simu nchini Norway wakati walipovamia jengo hilo.Mmoja wa washukiwa wa shambulizi hilo ametajwa kuwa Hassan Abdi Dhuhulow mzaliwa wa Somalia ingawa raia wa Norway.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...