ARSENAL, CHELSEA, BARCELONA ZAUA ULAYA

Wachezaji wa Arsenal Aaron Ramsey (kulia) na Mesut Ozil wakishangilia bao lao la pekee dhidi ya Dortmund. Bao hilo limefungwa na Ramsey dakika ya 62.
Mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o akishangilia na kocha wake Jose Mourinho baada ya kuifungia timu yake bao.
Lionel Messi (kushoto) akishangilia moja ya mabao aliyoifungia timu yake ya Barcelona na Cesc Fabregas.
Arsenal, Chelsea na Barcelona zimeibuka na ushindi katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizopigwa usiku huu. Arsenal wameilaza Borussia Dortmund bao 1-0, Chelsea wakiizamisha 3-0 timu ya Schalke 04 wakati Barcelona wakiichachafya AC Milan bao 3-1. Bao la Arsenal limefungwa na Aaron Ramsey ya Chelsea yakiwekwa kimiani na Samuel Eto'o aliyefunga mawili na Demba Ba wakati ya Barcelona yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga mawili na Sergio Busquets na lile la AC Milan Gerard Pique aliyejifunga.
(Picha zote: Reuters, AP na PA)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...