Mmoja wa wakazi wa mtaa huu aliyeamua kujitoa na kushika kinyesi ili apate kuzibua chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji bila kusimama kwa siku sita.
Hali hii ilikuwa mbaya jambo ambalo wananchi waliamua kujitolea na kufanya wawezalo ili kuzibua.
Hali
ni tete eneo hili ambapo sasa moja ya chemba inazidi kumwaga maji. Hapa
kila mtu anatoa wazo lake nini kifanyike ili kuweza kuzibua eneo hilo
ambalo maji yake yalikuwa hayapungui kumwagika bali kuongezeka na mwisho
wote waliona bora washike kinyesi kuliko kuendelea kuteseka.
Ilikuwa
ni baada ya kuhangaika sana wakazi wa eneo hili kwa kutumia nyenzo yao
duni ya nondo maalumu ya kuzibulia chemba waliyojinunulia wenyewe,
hatimaye walifanikiwa kuzibua chemba moja na kuhamia chemba ya pili.
Baada ya chemba ya juu kuzibuka, kasheshe ikahamia katika chemba ya pili ambapo sasa maji yote yalihamia hapo.
Masikini mtazame mama huyu alivyoruka juu na mtoto akiwa amemshika kihatari namna hii. Hii ni adha ya haya maji taka.
Wakazi wa eneo hili wakiwa wanakomaa kwa nguvu zote kuanza kuzibua chemba ya pili.
Zoezi
sasa linaendelea na hapa walikuwa wanaendelea kuzibua chemba ya 3
ambapo walifika kikomo baada ya kuonekana chemba hiyo ilikuwa imejaa
matakataka ya kutosha pamoja na mchanga. Ndipo walipopata taarifa kuwa
DAWASCO wanakuja.
Wakiwa wamefika kabisa na kujionea adha ya kukanyaga maji taka.
Wafanyakazi
wa DAWASCO wakiwa wamefika katika eneo la tatizo na kuanza kuzibua
chemba za maji taka ili kuwasaidia wakazi hao wasipatwe na magonjwa.
Wakiwa wanahakikisha kabisa kwamba tatizo limekwisha eneo hilo.
Mojawapo
ya chemba ambayo wakazi wa Mwenge walikuwa wamehangaika nayo sana mpaka
kufanikiwa kutoa maji taka hayo yaende ikiwa inaangaliwa na wafanyakazi
wa DAWASCO.
Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wanaendelea kutoa takataka katika chemba sugu ili kuruhusu maji yapite.
Hii ni baada ya chemba kuzibuliwa na wananchi wakishirikiana na DAWASCO ambao walichelewa kufika eneo la tukio.
Maji yakionekana yanaendelea kukauka baada ya chemba hizo kuzibuliwa.
Hizi ni takataka zilizobakia baada ya kuzibuliwa chemba hizo.
Wananchi mtaa wa Mwenge waandamana na kufanya usafi kufuatia kero
kubwa ilyokuwa sugu na hatari kwa afya zao, kero hiyo ikiwa ni kuziba na
kufumuka kwa chemba zinazopitisha maji machafu maarufu kama
(majitaka).
Ikiwa nizaidi ya wiki mbili wakazi na watumiaji wa njia ya Mwenge
katika mtaa huo uliogeuzwa jina na kupewa jina mahususi na mazingira ya
mtaa ambalo ni mtaa wa (kinyesi street) wamekumbwa na kero ya kufumuka
kwa chemba za maji taka na kuwa na harufu mbaya hivyo wananchi
wamehofia afya zao na kuanza kuzibua chemba za maji hayo huku kila baada
ya mwezi huletewa bili na kuweza kuzilipia bila ya wasiwasi. Lakini
kibao kimegeuziwa kwa wananchi kuwa ndio wamiliki wa shirika la maji
safi na taka (DAWASCO) baada ya kuamua kuondoa adha hiyo iliyodumu kwa
muda mrefu bila ya ufumbuzi kwa kushika kinyesi na maji machafu kutoka
sehemu mbalimbali.
Hata hivyo wakazi walilalamika kuhusu utendaji kazi wa DAWASCO kuwa ni mbovu kwa kuwa wamewatafuta zaidi ya mara kadhaa bila mafanikio.
Aidha wananchi walionekana kuwa na moyo mmoja wa ushirikiano kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka katika chemba hizo na kufanikisha kuzibua chemba zote katika mazingira magumu yanayoweza kusababisha maradhi mbalimbali kwa jamii husika.
(PICHA NA DAR ES SALAAM YETU)