HAFIDH KIDO APEWA USEMAJI COASTAL UNION YA TANGA

Msemaji mpya wa Coastal Union baada ya Edo Kumwembe.
Edo Kumwembe, pichani.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANDISHI na mdau wa karibu mno na timu ya Coastal Union ya jijini Tanga, Hafidh Kido, amefanikiwa kurithi mikoba ya msemaji wa zamani Edo Kumwembe kwa ajili ya kazi ya kupashana habari zinazoihusu klabu hiyo.
Akizungumza jana kwa njia ya simu akitokea mkoani Tanga, Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Aurora, alisema kuwa wamefikia uamuzi huo kwa ajili ya kuiweka nafasi hiyo kwa mtu makini na mwenye kuimudu zaidi. Alisema kuwa Kido alikuwa mdau wa Coastal huku akifanya kazi kwa karibu na Kumwembe wakati ni msemaji wa klabu hiyo, hivyo wanaamini kuwa atafanya kazi zake kwa moyo naa ujasili wa aina yake.
HABARI NA HANDENI KWETU


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...