RPC ILALA AITISHA KIKAO CHA MPANGO KAZI DHIDI YA UNYANYASI WA KIJINSIA

Kamanda wa Polisi, Marietha Minangi (katikati) akizungumza jambo mbele ya wadau.
Wadau mbalimbali wakiwa katika majadiliano.
                                                           Wadau wakimsikiliza kamanda Marietha.

KAMANDA  wa polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi, jana alifanya kikao na Dawati la Jinsia na wadau mbalimbali kupanga mpango kazi wa maadhimisho ya  siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Mkoa wa Ilala.
Akizungumza na wadau katika Ukumbi wa Polisi  wa Kituo Kikuu, Kamanda Marietha alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kushamiri katika mkoa wake hivyo kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 mwaka huu kutakuwa na maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutembelea watoto yatima na wenye mtindio wa ubongo walioko kwenye vituo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Tumia Mamlaka Yako, Zuia Ukatili wa Kijinsia, Boresha Afya ya Jamii’.
( STORI/PICHA: GLADNESS MALLYA NA HAMIDA HASSAN )


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...