WAWILI WAFARIKI, WAANGUKIWA NA UWANJA UNAOJENGWA BRAZIL KWA KOMBE LA DUNIA

Kikosi cha zimamoto kikimtoa mmoja wa watu waliokufa katika ajali hiyo.
Mandhari ya eneo la ajali.
Mashuhuda wa ajali wakitazama sehemu ya uwanja iliyoharibika.
Wafanyakazi wakisafisha eneo la ajali.
WATU wawili wanaamika kufariki baada ya kuangukiwa na sehemu ya juu ya uwanja  wa Sao Paulo ambayo ilisababishwa na kuporomoka kwa mashine yenye kubebea vitu juu (crane) wakati wa ujenzi wa moja ya viwanja vitakavyotumika katika fainali za soka Kombe la Dunia  huko Brazil mwaka kesho.
Sehemu ya mwisho ya uwanja huo ambao ni moja ya viwanja vyenye kuvutia katika fainali za mwaka 2014 ilikuwa inawekwa katika Uwanja wa Corithians ambapo mashine hiyo yenye uzito wa tani 500 ilipoporomoka na kusababisha uharibifu mkubwa.
Waliofariki ni  Ronaldo Oliveira dos Santos (44) na Fabio Luiz Pereira (42) waliokuwa katika eneo hilo.Mtu wa tatu ambaye amelazwa hospitali anasemekana hali yake ni mbaya.  Pia juhudi za kutafuta watu wengine waliohusika katika tukio hilo zilikuwa zinaendelea.

                                                            CHANZO NI DAILYMAIL


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...