WAZIRI WA ELIMU ATEMBELEA BANDA LA ATC MAONESHO YA KIMATAIFA YA MADINI

Waziri wa Elimu, Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea banda ya Arusha Technical College. Chuo hicho kinatoa mafunzo ya Uchakataji madini na kutoa wataalamu wanaokubalika katika soko. 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa akipokea Maelezo mafupi kuhusu Kozi ya Ukataji Madini na Utengenezaji wa Vito vya thamani kutoka kwa Bi. Shahzimin Premji alipotembelea banda la Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa akiangalia kwenye chombo maalum cha kupimia wakati alipotembelea Banda la Chuo cha Ufundi Arusha.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Richard Masika (Kushoto) alimkabidhi Waziri wa Elimu, Dkt. Shukuru Kawambwa moja wa Vito vya thamani vilivyochongwa na wanafunzi wanaosoma Kozi ya Ukataji madini Chuo cha Ufundi Arusha.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...