UKATILI,
unyama kila kona! Mariam Kilimba (52), mkazi wa Ipuli katika Manispaa
ya Tabora mkoani hapa anadaiwa kupigwa na mumewe hadi kuvunjwa taya.
Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni, mwanaume aliyetekeleza
ukatili huo ilielezwa kuwa ni mganga wa kienyeji na chanzo cha yote
hakikuelezwa mara moja kwani mwanamke huyo hajaweza kuzungumza.
Wakati tukio hilo likiacha wengi midomo wazi, huko Kata ya Isevya mkoani hapa mwanamke aliyetajwa kwa jina la Joha Aman (38) naye alipigwa na mumewe kisha kujeruhiwa vibaya.
Majeruhi wote hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Tabora Kitete huku watuhumiwa wakisakwa ili sheria ichukue mkondo wake.
Matukio ya ukatili wa kijinsia yanazidi kushika kasi kila kona ya nchi hivyo mamlaka zinazohusika zinaombwa kuchukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa.
GPL
Mariam Kilimba (52) aliyevunjwa taya na mumewe.
Wakati tukio hilo likiacha wengi midomo wazi, huko Kata ya Isevya mkoani hapa mwanamke aliyetajwa kwa jina la Joha Aman (38) naye alipigwa na mumewe kisha kujeruhiwa vibaya.
Joha Aman (38) akiuguza majeraha baada ya kuumizwa na mumewe.
Matukio ya ukatili wa kijinsia yanazidi kushika kasi kila kona ya nchi hivyo mamlaka zinazohusika zinaombwa kuchukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa.
GPL