Akizungumza na Pro -24 ,muda huu Madaha aliweka wazi kuwa wasanii hawatakiwi kuchukua kigezo cha kufanya ziara ndio kukua kimuziki na badala yake wanatakiwa wajipime na uwezo wao na jinsi muziki huo unavyosikika nje ya nchi.
Aliweka wazi kuwa kufanya ziara si sababu ya kumfanya msanii huyo kuonekana ameingia katika anga za kimataifa na badala yake wanatakiwa wajikite zaidi katika kuuza muziki huo kuhakikisha wanapata nafasi ya muziki wao kusikika katika nchi nyingin