MKUTANO
Mkuu wa Kijiji cha Olgilai wilayani Arumeru umeazimia kuwachapa viboko
vijana wa kiume wanaovaa suruali chini ya makalio pamoja na wanawake
wanaovaa sketi fupi na suruali zinazobana. Azimio hilo pia limeelekezwa kwa wanafunzi wanaopata mimba au kuozeshwa na kuacha masomo bila sababu za msingi.
wanaovaa sketi fupi na suruali zinazobana. Azimio hilo pia limeelekezwa kwa wanafunzi wanaopata mimba au kuozeshwa na kuacha masomo bila sababu za msingi.
Mkutano
huo umepitisha maazimio saba yanayolenga kurejesha nidhamu na heshima
kijijini Olgilai limefikiwa kutokana na vijana wa kike na kiume kuvaa
nguo zisizo na heshima.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Olgilai, Godson Boazi katika barua yake ya Januari 24
mwaka huu kwa viongozi wa makanisa kijijini hapo, aliwaomba kuunga mkono
hatua hiyo katika kurekebisha tabia ndani ya jamii yao.
“Viongozi
wa dini tunafahamu kazi kubwa ya kutunza kundi la Mungu likae kwenye
maadili mema. Hivyo basi tunaomba mtusaidie jukumu hili ambalo
tumeambatanisha barua kwenu,”alisema Boaz na kuongeza:
“Viongozi
wa dini tumewaandikia waraka huu tukijua kwamba ninyi ni watu muhimu
katika kusaidia jambo hili na kuwafikishia taarifa waumini wenu wote
wakubwa kwa wadogo.”
Katika
barua yake ambayo MTANZANIA inayo nakala yake Mwenyekiti huyo alisema
kwa kauli moja uongozi mkutano huo uliafiki suala hili na kuamuru lianze
kutumiwa Januari 24 mwaka huu.
Aliyataja
maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo
barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalumu watachapwa viboko.
Jingine
ni kuwachapa viboko wote watakaovaa nguo zisizofaa katika jamii yao
mfano sketi fupi, suruali zilizobana kwa wasichana na akina mama.
“Vijana
wa kiume wanaovaa suruali zinazojulikana kama mlegezo, uendeshaji ovyo
wa pikipiki, wavutaji wa bangi, dawa za kulevya, gongo na wanywaji wa
viroba, uchezaji kamari na karata.
“Wanaotukana
ovyo barabarani na kupiga kelele za uvunjaji wa amani, wezi wa vitu
vikubwa na vidogo kama kuku, ndizi, viazi, mahindi na mboga shambani
watashughulikiwa,” alisema Boazi.
Alisema
Mkutano Mkuu wa Kijiji ulijiridhisha kuwa matendo hayo yamechangia kwa
kiasi kikubwa kushuka kwa nidhamu kijijini hapo na maeneo mengine