Na Gladness Mallya na Hamida Hassan
KWA mara ya kwanza msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ amenaswa akiwa na mwanaume wa Kizungu anayedaiwa kuwa ndiye
mchumba wake.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mchumba wake.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, safari za mara kwa mara za
Shilole nchini Uingereza zimekuwa zikisababishwa na mchumba huyo wa
Kizungu ambaye huwa anamuita kufurahia penzi lao pamoja na kumtafutia
shoo mbalimbali.
“Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye
shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi
karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake,” kilisema
chanzo hicho.
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo.
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘upupu’ huo, mapaparazi wetu
walimtafuta Shilole ili aweze kufunguka ambapo bila kuumauma maneno,
alikiri kuwa amepata mchumba huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar.
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake huyo, Shilole alisema awali
walikutana kwenye moja ya shoo zake nchini humo ndipo urafiki ulipoota
mizizi na kufikia hatua ya kuwa wapenzi.
“Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa
napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu
yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda
ndipo tukaanzisha urafiki.
“Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum
alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita
nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole