Grace Simon mwenye miaka 14 anateseka na uzito.
GRACE Simon mwenye miaka 14 anateseka na uzito wa kupindukia wa kilo
111 (kama gunia moja la mahindi na viroba vitatu) hali iliyomsababishia
akatishwe masomo na walimu katika Shule ya Msingi Amani, Ukonga, Ilala
jijini Dar es Salaam alikokuwa anasoma.Grace ambaye mwaka huu angekuwa
darasa la saba lakini aliachishwa shule mwaka 2010 akiwa darasa la nne
na walimu wakimtaka akatibiwe.
MAMA MZAZI ASIMULIA
Akizungumza na Uwazi kuhusu mkasa mzima wa mtoto Grace, mama yake mzazi,
Ashura Bakari alisema binti yake alimzaa salama mwaka 2000 lakini
ilipofikia mwaka 2002 akiwa na miaka miwili alianza kuvimba tumbo hali
ambayo hakujua chanzo chake.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
ATENGWA NA WANAFUNZI
Mama huyo akizungumza kwa masikitiko alisema kuwa, Grace alipofika
darasa la nne, akiwa na umri wa miaka kumi baadhi ya wanafunzi wenzake
walianza kumnyanyapaa kutokana na unene ambao ulikuwa ukiongezeka siku
hadi siku.
“Walikuwa wakimtania sana mwanangu hadi kukosa amani. Hali hiyo
iliwafanya walimu kumsimamisha masomo ili atibiwe. Hadi sasa sijapata
msaada wa kupona kwake,” alisema mama huyo huku machozi yakimtoka.
HOSPITALI ZIMESHINDWA?
Aidha, mama Grace aliongeza kuwa amekwishahangaika katika hospitali
mbalimbali za jijini Dar es Salaam, ikiwemo Muhimbili bila mafanikio.
“Muhimbili waliniambia ili mwanangu aweze kufanyiwa vipimo pamoja na
matibabu gharama zake ni shilingi laki nane (800,000) ambazo nimezikosa
na hakuna mtu wa kunisaidia,” alisema.
NDUGU NAO
Alisema mbali na kutafuta tiba hospitalini, amekuwa akipita huku na huko
kuomba msaada wa fedha kutoka kwa ndugu na jamaa lakini hakuna
aliyemsadia.
KWA NINI BABA MZAZI ASIMSAIDIE?
Katika hali ya kushangaza, mama huyo alisema ili kupata fedha hizo
anahangaika peke yake kwa sababu baba mzazi wa Grace, Simon alikataa
kutoa msaada wowote.
“Baba yake yupo hai, alikuwa anatoa msaada kipindi cha mwanzo lakini
miaka kama mitano imepita hakuna msaada anaonipa. Ni kweli hatuishi
pamoja lakini mtoto tulizaa wote,” alisema kwa masikitiko makubwa mama
huyo.
WALICHOKIONA MADAKTARI
Akizungumzia kiini cha tatizo, mama huyo alisema: “Kwa mujibu wa
madaktari mwanangu anasumbuliwa na moyo kujaa mafuta mengi, kwa hiyo
homoni zake zimekosa uwiano na ini pia lina sumu nyingi.”
GRACE AWALILIA WATANZANIA
Akizungumza na mwandishi wetu, mtoto huyo anayetamani kuendelea kusoma
aliwaomba Watanzania wamsaidie fedha ili aweze kutibiwa na kurejea
darasani.
“Niliachishwa shule ili nitibiwe, nikipona nirejee shuleni, lakini hadi
sasa sijapata nafuu, na ninajua ni kutokana na kutopata matibabu
sahihi,” alisema Grace huku akilia.
UONGOZI WA SHULE
Mmoja wa walimu waandamizi wa Shule ya Msingi Amani alipokuwa akisoma
mwanafunzi huyo (hakuwa tayari kutaja jina lake), alikiri kumtambua
mwanafunzi huyo na kusema aliachishwa shule kwa hofu ya uongozi wa
shule.
“Hatukumwachisha shule kwa nia mbaya, lakini lengo letu lilikuwa
akatibiwe kisha arudi shuleni lakini matibabu anayopata hajaweza kupona
na hali aliyokuwa nayo inazidi kuongezeka siku hadi siku,” alisema
mwalimu huyo.
Akaongeza: “Mwaka huu Grace ilikuwa awe darasa la saba, lakini hata
kutembea ni tatizo hali ambayo tuliona kuwa unene ule si afya bali ni
ugonjwa.”
MSAADA UNAAOHITAJIKA
Kwa
yeyote aliyeguswa na tatizo la Grace ambaye anasaka shilingi laki nane
tu ili atibiwe, anaweza kuwasiliana na mama yake mzazi kwa simu: 0719
465445, ASHURA BAKARI.
CHANZO GLOBAL PUBLISHERS