MWANAMKE ANASWA AKITAKA KUMTOROSHA BINTI

Stori: Francis Godwin, Iringa
WAKAZI wa Kitongoji cha Frelimo mkoani hapa wamemkamata mwanamke aitwaye Zuhura Angero kwa madai ya kutaka kumtorosha binti wa kazi, Felenesta kwa ajili ya kumpeleka jijini Dar es Saalam kufanya kazi za ndani.
Zuhura Angero (kulia) akiwa na binti aliyetaka kumtorosha.
Tukio hilo la aina yake limetokea saa mbili usiku Januari 12, mwaka huu baada ya wakazi hao kumwekea mtego mwanamke huyo na kumnasa.
Inadaiwa kwamba mwanamke huyo ambaye ni mwenyeji wa Iringa aliyehamia Dar, alifikia nyumba ya jirani na anapoishi Felenesta ili iwe rahisi kumtorosha  binti huyo usiku huo.
“Baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa msichana, tulimwambia amwite mwanamke huyo nyumbani na kumweleza kwamba alikuwa peke yake  na alipofika tukamweka chini ya ulinzi,” kimesema chanzo chetu kilichokuwepo eneo la tukio.
 
Zuhura Angero baada ya kunaswa.
Baada ya kumnasa, mwanamke huyo alikiri kutaka kumchukua Felenesta na kumpeleka Dar, hivyo akatakiwa kukiri kwa maandishi chini ya vijana wa polisi jamiii.
“Pamoja na kukiri tulimtaka kuandika maelezo iwapo msichana huyo akipotea yeye ataingia matatani kisha tukamwachia,” kimeendelea kudai chanzo hicho.
Katika maelezo yake, Felenesta  alidai kwamba mwanamke huyo alimwambia angekuwa na maisha mazuri iwapo angefika Dar kwani amewasaidia wengi.
Mkoa wa Iringa umepiga marufuku vitendo vya baadhi ya watu kuwachukua wasichana, wavulana na kuwapeleka Dar es Salaam kwa ajili ya kufawanyisha kazi za ndani.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...