WATANGAZAJI
maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi
‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, wamepigwa chini na
kituo hicho, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo alikiri.
“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.
GPL
Hamis Mandi ‘B 12’.
Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa
uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya
utovu wa nidhamu wa watangazaji hao.Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo alikiri.
Adam Mchomvu.
“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu
baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo
kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo
hazikutarajiwa.“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.
Loveness Malinzi ‘Diva’.
Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema:
“Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao
watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati
tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na
tulivyokubaliana.”GPL