MARIAMU
HUSSEIN akiwa na hali mbaya baada ya kuchomwa kisu mgongoni na kwenye
paja wakati alipovamiwa na mwanamke mmoja ambaye inadaiwa kuwa Mariamu
alikuwa na mahusiano ya kimapenzi
na mume wa mwanamke huyo.Katika mkasa huo ilielezwa kuwa Mariamu akiwa
nyumbani kwao ghafla alifika mwanamke huyo na kudai kuwa amekuja
kutekeleza
mauaji kwa kile kilichofahamika kuwa amekuwa akivumilia kwa muda mrefu
kuchukuliwa mume wake pasipo kuleta fujo yeyote jambo ambalo lilionesha
unyonge wa hali ya juu kwa mwanamke huyo ambaye alifika nyumbani hapo na
kucharuka kama Mbogo aliyejeruhiwa na kuanza kufanya unyama huo.
Mwanamke
aliyefanya unyama huo,alilazimika kukimbizwa Kituo Kikubwa cha Polisi
Tabora,...Mariam akiwa hoi taabani huku damu ikiendelea kububujika
kwenye jeraha kubwa la mgongoni.
Mpini
wa kisu alichochomwa Mariamu ambapo inasadikiwa Mwanamke huyo baada ya
kumpiga kisu cha mgongoni na kuingia,kilikatikia mgongoni na kumfanya
Mariamu azidiwe na kupoteza fahamu