ISSUE YA KUKACHA KANISA:. KIONGOZI WA KANISA AMKINGIA KIFUA JOKATE
KIONGOZI
wa kwanya katika Kanisa la St. Peter, Oysterbay jijini Dar, Rogers
Mgonja amemtetea mwanamitindo mahiri Bongo, Jokate Mwegelo kuwa
hajalikacha kanisa kama inavyodaiwa.
Mwanamitindo mahiri Bongo, Jokate Mwegelo
Hivi karibuni ziliibuka taarifa kuwa, Jokate amezuiwa kutinga
kanisani hapo kutokana na kuvaa mavazi ya nusu utupu yasiyoendana na
maadili.
“Jokate
ni mwanadada mwenye nidhamu sana kanisani, viongozi wote wanampenda ni
mpole na msikivu, Kama ni mavazi, kanisani anavaa mavazi ya heshima ni
ngumu sana kumfukuza kwa sababu ambazo haziingiliani na masuala ya
kanisa,” alisema Mgonja