

Matic ambaye anarejea Chelsea baada ya kuihama akiwa ni sehemu ya
uhamisho wa beki David Luiz,amesajiliwa tena kwa mkataba wa miaka 5 na
nusu kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 21.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 tayari amekabidhiwa jezi namba 21.