TAZAMA PICHA::KIJANA ANUSURIKA KUUAWA KARIAKOO BAADA YA KUKWAPUA POCHI YA MWANAMAMA

 Hapa ni wanainchi wenye hasira kali wakitaka askari wamuachie kibaka huyo ili wamwadabishe
 Huyu ndio kibaka aliyeokolewa na Polisi kutoka kwenye mikono ya wanaichi wenye hasira kali sana
 Wanainchi wakiwa bao wanalazimisha kibaka huyo atolewe ili wamwadhibu
 Ohhhh siamini kama nimepona kwa kipigo toka kwa hawa wanainchi
wanainchi wakijipatia ukodak wa tukio
Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amenusurika kipigo  kutoka kwa wanainchi wenye hasira kali eneo la msimbazi kariakoo mchana wa leo.Chanzo cha tukio hilo ni pale kijana huyo alipokwapua pochi ya mama mmoja na kuanza kukimbia ndipo wanainchi wakamuungia na kuanza kushinda marathon.Baada ya kijana huyo kuona timu ya marathon iliyo nyuma yake ni kubwa na ya kutosha akaamua kujisalimisha kwenye kibanda cha askari wa usalama barabarani wanapatikana eneo la around about ya msimbazi.

Wanainchi walifika eneo hilo na kutaka polisi wamwachie kijana huyo ili wamwahibu lakini polisi walisisitiza lazima sheria zifuatwe hivyo basi wanainchi wasivunje sheria kwa kumpiga.Mpaka Dj sek blog inaondoka eneo la tukio kijana huyo alikuwa chini ya ulinzi wa polisi.Rai ya mtandao wetu jamani wakina dada na wakina mama kuweni makini kuweni makini na hivyo vipima joto vyenu na pochi zenu za mikononi,huu mwanzo wa mwaka watu wana njaa jamani.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...